Na: Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini (H/W) Masasi.
Matukio katika picha.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ndanda na Lulindi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndg.Keneth Mgina amekabidhi fomu ya Uteuzi kwa mgombea Ubunge Jimbo la Lulindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Ali Issa Mchungahela.
Zoezi hilo la utoaji wa fomu linafanyikia katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ndanda na Lulindi zilizopo Mbuyuni Masasi .
Ifahamike kuwa, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani lilianza rasmi Agosti 14 na litahitimishwa kesho tarehe 27 Agosti 2025.
"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura "
26/08/2025.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa