Wakuu wa Idara, Vitengo pamoja na Wasaidizi wao Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wamepatiwa Mafunzo ya Mfumo wa Kielektoniki wa Ukaguzi na Ufuatiliaji Fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (IFT-MIS).
Mfumo huo umelenga Kurahisisha Uandaaji wa Mpango Kazi kwa Kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Bw. Shedrack Mbago ni Afisa TEHAMA Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambaye ni miongoni mwa Wawezeshaji wa mada kuu ya Matumizi ya Mfumo wa IFT-MIS kwenye ngazi ya Halmashauri amesema kuwa wanatoa Mafunzo hayo ili kuendelea kuwajengea uwezo wa namna ya kujibu hoja mbalimbali zitakazojitokeza kwenye Idara zao kwa hutumia Mfumo maalumu ulioletwa na Serikali kupitia TAMISEMI ujulikanao kama IFT-MIS.
"Upo umuhimu mkubwa wa Wataalamu hawa, kupitia Mafunzo haya tunayowapatia kushirikiana sasa kwa karibu na Ofisi za Mkaguzi wa Ndani na wahusika wengine wakati wa kujibu hoja na kuhakikisha zinafungwa kwa wakati."alisisitiza BW.Shedrack
Mafunzo hayo ambayo yameongozwa na Kitengo cha Ukaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kushirikiana na Maafisa TEHAMA pamoja na mhasibu wa Hoja yamefanyika mapema Tarehe 09 -10 /05/2025 katika Ukumbi wa zamani wa Halmashauri hiyo uliopo Masasi Mjini .
11/05/2025.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa