WAKUU WA DIVISHENI, VITENGO NA MAAFISA BAJETI
Wakuu wa Divisheni, Vitengo na Maafisa bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo ya uandaaji wa mipango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 huku wakisisitizwa kuhakikisha vile vipaumbele muhimu vya Maendeleo kwa ajili ya Halmshauri vinawekwa katika mipango yao.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndg.Alphaxard Etanga wakati akifungua mafunzo hayo ya siku moja kwa maafisa hao ambapo pamoja na mambo mengine amebainisha mambo kadhaa ya kuzingatia ikiwemo miongozo ya mipango na bajeti inayotolewa kila mwaka kwa kuzingati Dira ya Taifa ya Maendeleo, Mpango wa Taifa wa maendeleo wa muda wa kati na sera za kitaifa.

"Nyinyi maafisa bajeti wa Halmashauri nawaomba sana, mnapokuwa mnaandaa bajeti zenu zingatieni taratibu zote muhimu katika uandaaji wa Mipango na bajeti ili kuleta matokeo mazuri yatakayorahisisha utekelezaji wa mpango katika shughuli za kila siku, mimi mara kwa mara nimekuwa nikiwaambia wakuu wa idara wakae na wataalamu wao kwa pamoja mshirikiane kuona ni vitu gani ambavyo vinatukwamisha kwenye bajeti zetu ili virekebishwe, mzingatie sasa uwazi na usahihi wa malengo, shabaha na hasa yale maeneo muhimu ya vipaumbele na shughuli husika zitakavyotekelezeka kwa Halmashauri wekeni katika mipango na bajeti zenu ili kuonyesha uhalisia wa Taasisi ilipo, mwelekeo na kusudio tarajiwa"... alieleza Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Idara ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bw.Godfrey Makenzi amesisitiza umuhimu wa kuzingatia uchaguzi wa malengo kwa kuzingatia mpango wa bajeti na kuhakikisha shabaha zinazowekwa zinatekelezeka.

"Uandaaji wa mipango na bajeti ya Serikali ni muhimu kwa sababu ndiyo nyenzo kuu ya kusimamia mipango ya Maendeleo na matumizi ya rasilimali za Serikali, hivyo mipango na bajeti moja kwa moja huonyesha vipaumbele vya Serikali kwa mwaka husika katika sekta mbalimbali kama afya elimu, utawala na miundombinu "..alifafanua zaidi Mwezeshaji huyo.

Mafunzo hayo siku moja yaliyofanyika mapema tarehe 18 Novemba 1025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo Mbuyuni Masasi, yamehudhuriwa na maafisa bajeti kutoka Divisheni na Vitengo vyote, sambamba na maafisa kutoka Hospitali, zahanati na Vituo vya Afya vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa