Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 leo tarehe 19/05/2025 Umetembelea jumla ya Miradi mitano (5) yenye thamani ya Shilingi Milioni 678,844,040.00 katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Kati ya miradi hiyo, mradi mmoja (1) umewekewa jiwe la msingi, mradi mmoja (1) umefunguliwa, mradi mmoja (1) umezinduliwa na miradi miwili (2) imekaguliwa, kuonwa na kupata taarifa.
Mwenge huo ambao umekimbizwa umbali wa kilomita 104.1 umepita katika Vijiji 21, Kata 6 na Tarafa 2.
Moja ya Miradi ambayo umefunguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ni Mradi wa Jengo la Mionzi la Kituo cha Afya Chiwale (X- ray) ambapo Halmashauri kupitia Mapato yake ya ndani ilitoa fedha kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza ni Shilingi Milioni 50,000.000.00 tarehe 01/02/2024, awamu ya pili ni Tsh.milioni 50,000,000.00 tarehe 19/09/2024, awamu ya tatu Tsh.milioni 30,000,000.00 tarehe 12/11/2025 na awamu ya nne Tsh.milioni 15,000,000.00 tarehe 14/02/2025.
Mradi mwingine ambao umezinduliwa na Mwenge huo ni Jengo la Elimu ya Awali Shule ya Msingi Chikukwe, lenye vyumba 2 vya Madarasa na matundu ya vyoo sita, ambapo Serikali imetoa kiasi cha Tshs Milioni 67,300.000.00 huku nguvu za Wananchi ni Shilingi Milioni 300,000.00 ( kuchimba msingi na kusogeza tofali eneo pa ujenzi).
Uwekaji jiwe la Msingi umehusisha Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Nazareti- Pachani (0.8 km) kwa kiwango cha lami Kata ya Chiwale, ambapo umeendelea kutoa ajira kwa Viķundi maalumu vya akina mama, mama lishe na Vijana, vilevile mradi huu ukikamilika utapunguza gharama za matengenezo ya barabara zilizokua zikutumika kila mwaka.
Aidha mradi huu unatekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo na mkandarasi mzawa, ambapo gharama ya mradi huu ni Tsh.milioni 450,569,750.00 hadi kukamilika kwake.
Mradi mwingine ulioonwa na kukaguliwa ni Shamba la miti Ndanda pamoja na kuona na kukagua shughuli za Vijana za ufyatuaji tofali za Kikundi cha Mashujaa- Tuungane.
Mwenge wa Uhuru pia umeona na Kukagua shughuli za Uchaguzi Mkuu, Kongamano la Vijana, Kuona na Kukagua banda la Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria na dawa za kulevya, kuona na kukagua banda la afua za lishe, kuona na kukagua shughuli za Mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa Kijinsia,Risala ya utii, ujumbe wa Mwenge wa Uhuru na mkesha.
19/ 05/ 2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa