Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya ( Mama Samia Legal Aid) ikiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi leo Alhamis tarehe 30/01/2025 imeendelea kutoa huduma za Kisheria bure kwa Wananchi mbalimbali Kwa lengo la Kutatua Migogoro mbalimbali inayowakabili ili kuimarisha Ustawi wa Jamii na Usawa katika Taifa.
Aidha watendaji wa Kampeni hiyo pamoja na kutoa elimu mbalimbali lakini pia wakapata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Mwananchi mmoja mmoja kwa kusikiliza changamoto zao zinazowakabili na hatmaye ziweze kushughulikiwa .
Hata hivyo kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka kijiji cha Chikunja,Nanditi, Napata, Mraushi,Lukuledi A na Lukuledi B, ambao wamefikiwa na huduma hiyo kwa siku ya leo tarehe 30/01/2025 wamemshukuru mhe.Rais Dokt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwasogezea huduma hiyo katika ngazi ya chini kabisa ambapo wanaelimishwa na kupewa miongozo mbalimbali ya Kisheria na namna ya kufanya wanapokutana na changamoto zinazohitaji msaada wa kisheria.
30/01/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa