Wito umetolewa kwa Watumishi wa Umma kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri na kuziba mianya ya utoroshaji wa mapato.
Wito huo umetolewa mapema leo tarehe 04/09/2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndg.Alphaxard Etanga wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mbuyuni Masasi.
Amesema ili Halmashauri iweze kuwalipa stahiki wafanyakazi inategemea kukusanya mapato ya ndani , hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kwa nafasi yake anatakiwa kuhakikisha mapato ya ndani yanakusanywa na kulindwa.
“Suala la kukusanya mapato ya ndani ni la kwetu sote watumishi, na hakuna anayependa mtumishi asilipwe stahiki zake, kila mtumishi popote alipo ahakikishe anakusanya mapato na kuziba mianya ya kutorosha mapato”,alisema.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya ya usimamizi katika ukusanyaji mapato ya ndani hivyo lazima waendelee kushirikiana kwenye vita hiyo ya uchumi ili Halmashauri iweze kuvuka lengo la ukusanyaji mapato.
"Naomba kila idara ikae na kujadili suala la mapato kwasababu nanyi ni sehemu ya mapato, tukague POS zetu,tudhibiti mapato yetu, tukague leseni za biashara, tukague katika mageti na kuweka ulinzi pia".alisema.
04/09/2025.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa