Na.Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini (HW) Masasi.
Timu ya Menejimenti (CMT) ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Leo tarehe 09/07/2025 imefanya Ziara ya Kutembelea na Kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kupitia fedha kutoka Serikali kuu na Wahisani.
Timu hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Keneth Mgina ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha huduma za Sheria amesema ziara hiyo ni moja ya utaratibu ambao kama Halmashauri umejiwekea wa mara kwa mara kutembelea Miradi ya Maendeleo pamoja na kubaini zile changamoto ambazo zimejitokeza wakati wa utekelezaji wa Miradi hiyo na hatmaye kuzitatatua kwa wakati.
Akizungumza na Wasimamizi wa Miradi pamoja na baadhi ya Mafundi ujenzi ambao wamewakuta katika Miradi hiyo wanayoitekeleza, Kaimu huyo amewasisitiza kuongeza jitihada ili wakamilishe Miradi kwa wakati na ubora unaoendana na thamani ya fedha iliyotolewa na hatmaye iweze kuleta tija sambamba na kuzingatia mikataba yao.
Miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa Kituo cha Afya Namajani, Ujenzi na Ukarabati wa Stendi ya Mabasi-Ndanda, Mradi wa Kuendeleza ujenzi wa Soko la kijiji cha Chigugu, Ujenzi wa matundu ya vyoo nane(08) vya Wanafunzi Shule ya Msingi Mwongozo , Mradi wa Choo na Kichomea Taka Zahanati ya kijiji cha Mlingula, Ujenzi wa Darasa moja na Ukamilishaji wa chumba kimoja cha darasa Shule ya Msingi Mpowora, Umaliziaji wa Nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Sekondari Mbemba, Ujenzi wa Miundombinu ya maji na usafi katika Zahanati ya Nasindi pamoja na ukamilishaji wa vyumba 4 vya Madarasa Shule shikizi ya Sululu ya leo.
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inaendelea kusimamia utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezai ambapo siku ya kesho tarehe 10/07/2025 ni siku ya pili ya ziara hiyo huku Menejimenti ikitarajia kutembelea na kukagua Miradi kwenye Jimbo la Lulindi.
09/07/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa