TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA ROBO YA PILI (OKTOBA – DISEMBA), 2017.
Mhe. Mwenyekiti,Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Halmashauri ilipanga kutekeleza miradi ya maendeleo yenye thamani ya fedha Shs. 7,645,346,600.00 kati ya hizo; Shs.3, 752,900,000.00 ni fedha za ndani (Serikali Kuu) na Shs 958,227,000.00 ni fedha za nje (Wahisani), na Shs. 2,934,219,600.00 ni fedha za Mapato ya Ndani.
Katika kipindi cha Julai 01, 2017 hadi Disemba 31, 2017, jumla ya shs. 1,780,652,427.73 zimepokelewa ambayo ni sawa na asilimia 23.29 ya bajeti yote ya Miradi ya Maendeleo. Fedha zilizopokelewa ni kwa ajili ya Ujenzi wa Ukumbi na Ofisi za Halmashauri Tshs. 200,000,000.00, Mfuko wa Jimbo shs. 76,975,000.00, Elimu bila malipo Msingi shs. 404,518,908.00, Elimu bila malipo Sekondari shs. 488,143,529.79, Mradi wa UNICEF shs.121, 260,890.00, Mfuko wa pamoja wa Afya shs.123, 534,400.00, Mapato ya Ndani ya Halmashauri shs. 322,219,600.94 na Ruzuku ya usambazaji maji vijijini sh. 44,000,000.00
Pia Halmashauri imepokea shs. 4,976,737,634.84 Fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo ambazo hazikuwepo kwenye Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/2018. Fedha hizo ni kwa ajili ya Miradi ya TASAF shs. 1,977,858,751.59, Mfuko wa Maji vijiji shs. 1,435,052,639.25, Delloitte shs.16, 145,000.00, Mfuko wa maendeleo ya Wanawake na Vijana shs. 16,000,000.00, Magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTD) shs. 65,881,294 na Mpango wa kuboresha vituo vya Afya shs. 400,000,000.00, Ujenzi wa miundombinu shule ya msingi Chiwata sh. 86,600,000.00, ujenzi wa miundombinu shule ya msingi Chidya sh.86, 600,000.00, Ujenzi wa miundombinu shule ya Sekondari Ndwika sh. 400,000,000.00, Ujenzi wa miundombinu shule ya sekondari Chidya sh. 400,000,000.00 na Ujenzi wa miundombinu shule ya Msingi Nairombo sh.66,600,000.00
Hivyo kufanya jumla ya Fedha zote zilizopokelewa nje ya bajeti kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha kuanzia Julai 01, 2017 hadi Disemba 31, 2017 kuwa shs. 6,731,390,062.57, kati ya hizo Shs. 4,571,545,480.22 zimetumika sawa na asilimia 67.91 ya fedha zilizopokelewa.
Pia katika kipindi hiki cha Julai 01, 2017 hadi disemba 31, 2017 Halmashauri imeendelea kutekeleza miradi ya mwaka 2016/2017 yenye thamani ya shs.148, 085,085.49 kwa fedha za BAKAA ambapo hadi Disemba 31, 2017 jumla ya shs. 123,315,335.78 zimetumika sawa na asilimia 83.27 ya fedha zilizovuka mwaka wa fedha 2016/2017.Bofya hapa kuona miradi iliyopangwa kutekelezwa.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa