Shule ya Msingi Mnavira ipo katika kijiji cha Mnavira Kata ya Mnavira. Shule hii ni miongoni mwa Shule tatu za Msingi zilizopo katika Kata hii. Shule in jumla ya wanafunzi 612, wakiwemo wavulana 315 na wasichana 297. Shule ina Walimu 7, wote wakiwa ni wa kiume.
Shule ya Msingi Mnavira ina mahitaji ya vyumba vya madarasa 15, vyumba vilivyopo hadi sasa ni 8, na upungufu ni vyumba 7. Mapema mwaka 2016, Kamati ya Shule kupitia vikao vyake vya kawaida na baadaye Mkutano Mkuu wa Kijiji waliamua kutafuta namna ya kupata fedha kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa vitatu ili kupuguza upungufu huo. Vyumba hivi vikikamilika upungufu utakuwa ni vyumba vinne. Kutokana na jitihada hizi tunaamini tatizo litaendelea kupungua.
Katika jitihada hizo za kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa haya, baadhi ya wananchi walitoa Mashamba yao ya Mikorosho na kuikabidhi Shule ili iweze kuyahudumia, kitendo ambacho kiliiwezesha Shule kupata mapato kupitia mauzo ya Korosho na hivyo kupata mapato yaliyowezesha ujenzi wa madarasa haya hadi kufikia Linta.
Ujenzi wa vyumba hivi vitatu vya madarasa kwa kutumia nguvu za Wananchi ulianza mwezi Desemba 2016, ambapo wananchi waliweza kujitolea kuchimba Msingi, kusomba mchanga na kazi zingine za kiufundi.
Hadi kufikia hatua hii ya ujenzi, jumla ya Tshs 29,480,000 zimetumika kwa mchanganuo ufuatao;
Ujenzi wa vyumba hivi utasaidia kupunguza/kuondoa mapungufu ya jumla ya vyumba 7 na hivyo kubaki na uhitaji wa vyumba 4.
Vyumba vitatu vya madarasa
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa