UJENZI WA MRADI WA MAJI WA SHAURIMOYO MPINDIMBI WENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.7
UJENZI WA MRADI WA MAJI WA SHAURIMOYO MPINDIMBI WENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.7
Mradi wa maji wa shaurimoyo mpindimbi ni kati ya miradi ya maji inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya masasi. Mradi ulinza kuteelezwa mwaka 2013 kwa gharama ya mradi ni Tsh 1,700,000,000.00
Hadi sasa mradi umefikia asilimia 90 ambapo kazi za ujenzi wa matenki, ulazaji mabomba na ujenzi wa vigawa maji umefanyika kwa asilimia kubwa na sasa iko hatua ya umaliziaji. Mradi unatarajia kukamilika julai mwaka 2017.
Katika kutekeleza mradi huu halmashauri imechagia asilimia 2.5 na wananchi wamechangia asilimia 2.5 huku serikali kuu ikichangia asilimia 95.
Mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 936,123,000.00 zimeshatumika.
Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia wananchi kupata maji yenye uhakia na hivyo kuondokana na tatizo la maji kabisa.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa