• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ZOEZI SHIRIKISHI NA HARAKISHI DHIDI YA CHANJO YA UVIKO-19 LASHIKA KASI MASASI DC

Posted on: September 25th, 2021

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Joshua Sanga akizindua Mafunzo ya zoezi la Mbinu Shirikishi na Harakishi la Chanjo ya Uviko-19 awamu ya pili amewataka wadau kuendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali kupitia vikao vya kamati za msingi za afya, kwenye Halmashauri, sambamba na kwenda kwa wananchi kufanya mikutano ya vijiji na Mitaa,  kutoa ufafanuzi na maelekezo sahihi  kwa baadhi ya makundi ya watu wenye imani potofu dhidi ya chanjo ya ugonjwa wa uviko-19. 

Hata hivyo Timu za Uhamasishaji ziliweza kufanya vikao katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri kwa ajili ya kutoa Hamasa kwa wananchi ambapo makundi mbalimbali yalihusishwa wakiwemo Viongozi wa Dini, Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Watu Maarufu na Wenye ushawishi ndani ya Jamii, Waheshimiwa Madiwani pamoja na wauguzi wa Afya kutoka Vituo mbalimbali vya Kutolea huduma lengo likiwa ni kutoa Elimu na Hamasa kwao ili Elimu ambayo wataipata wakaiambukize katika jamii na maeneo yao wanakoishi ,

Akaendelea kusema “Kuanzia tarehe 01 Oktoba 2021   wataalam wapite nyumba kwa nyumba na maeneo yenye mikusanyiko sokoni, stendi na sehemu zinazotoa huduma mbalimbali ikiwepo kwenye Misikiti na makanisa kwa siku za ijumaa na jumapili na  kutoa huduma za chanjo kabla na baada ya ibada, huku wakizingatia namna rahisi ya utoajiwa  chanjo kwa haraka bila ya foleni ili kurahisisha zoezi hilo.

Mwisho kabisa Kaimu Mkurugenzi  amewataka wananchi wote katika Halmashauri ya WIilaya ya masasi  na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo kuanzia tarehe 01 Oktoba 2021 itakuwa inapatikana katika Vituo vyote vya kutolea huduma  yaani kuanzia ngazi ya zahanati zote, Vituo vya Afya, pamoja na Hospitali  jambo ambalo litawezesha wananchi wengi kufanya kazi zao kwa uhuru bila ya woga wa virusi vya UVIKO-19 na kujenga Uchumi wa Familia zao na Taifa kwa Ujumla..

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mtwara ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Masasi kwa mapokeo mazuri ya chanjo ya UVIKO 19 katika mkoa huo, Mkoa wa Mtwara hadi kufikia siku ya leo umekuwa mstari wa mbele kwa kufikia asilimia 85  ya chanjo ya UVIKO 19  kati ya dozi 20,000 zilizokuwa zimepokelewa tokea Julai, 28,2021 kwenye Mkoa  huo.

Amesema kuwa, katika kuhakikisha asilimia 15 za dozi zilizobaki zinakamilika fursa za chanjo zitolewe kwa wananchi hususani kwa maeneo ambayo yalibainika kuwa chini katika uchanjaji.

Katika kufanikisha zoezi hilo Gaguti amesisitiza kuwa, katika zoezi Shirikishi na Harakishi linalo endeshwa na Serikali kwa sasa, ni vizuri kila mtu ambaye bado hajajitokeza, aweze kujitokeza apate elimu na akielimika aweze kupatiwa chanjo ya UVIKO 19.

Pichani ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya akitoa neno juu ya zoezi la uchanjaji  wa Uviko-19 wakati wa Mafunzo hayo kwa niaba ya Wizara yaliyolenga kuwajengea uwezo wauguzi wa Afya katika Vituo vya kutolea huduma mbinu shirikishi na Harakishi kwa wanachi  dhidi ya chanjo ya Uviko-19 katika awamu ya pili.

Pichani ni Afisa Tehama wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Ndugu Shedrack Omary akitoa maelekezo kwa wauguzi wa Vituo vya Afya juu ya matumizi ya Mfumo wa kutuma Maombi ya Chanjo ya Uviko-19 ambapo maombi yote ya chanjo na taarifa mbalimbali zitakuwa zinafanyika kupitia mfumo huu ambapo muombaji atatakiwa kuwa na namba za kitambulisho kama vile kitambulisho cha mpiga kura, Nida, Passport, au Leseni wakati wa kuomba  na mwisho wa zoezi muombaji atapata cheti maalumu ambacho ni Online certificate  yenye Barcode ambacho kitamtambulisha Dunia nzima.Tuma maombi yako sasa kupitia link hii... https://chanjocovid.moh.go.tz/


Pichani ni washiriki wa idara ya Afya kutoka katika Vituo mbalimbali vya Kutolea Huduma katika Mafunzo Maalumu ya Mbinu Shirikishi na Harakishi dhidi ya Utoaji wa Chanjo ya Uviko-19 katika awamu ya pili.

Washiriki wa Semina elekezi juu ya Chanjo ya Uviko-19 wakiwa makini kusikiliza na kufuatilia hatua kwa hatua somo hilo, ambapo mada mbalimbali ziliweza kuwasilishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wauguzi wa Afya kutoka katika Vituo mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya Halmashauri ya Wilaya Masasi.


KORONA IPO NA INAUA TENA KWA KASI

CHUKUA HATUA NENDA KACHANJE LEO

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa