Katika kutekeleza Afua za mapambano dhidi ya malaria, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa kugawa vyandarua vyenye viuatilifu 75,886 kwa wajawazito, watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaopata chanjo ya surua ya kwanza, na watoto shule za msingi kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la saba.
Hatua hiyo imefanya idadi ya wagonjwa wa malaria wanaokwenda kutibiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kupungua kutoka asilimia 5.5% sawa na wagonjwa 12710 mwaka 2022/2023 na kufikia asilimia 3.2% sawa na wagonjwa 2130 mwaka 2023/2024.
Pia maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa mama wajawazito yamepungua kutoka asilimia 4.6% mwaka 2022/2023 na kufikia asilimia 3.4 mwaka 2023/2024.
Kufuatia taarifa hiyo ya mapambano dhidi ya Malaria iliyosomwa na Mratibu wa Malaria wa halmashauri ya Wilaya ya masasi Dkt.Kazibure Juma kwa mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Ndg.Godfrey Eliakimu Mzava na ndipo ikapatia fursa ya kutembelea banda na kuona miongozo,dawa na vitendanishi kwa ajili ya matibabu ya malaria na kisha kugawa vyandarua kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 waliopata chanjo ya surua ya kwanza.
Kazi iendelee!..
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa