Uongozi wa Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma Leo tarehe 12/02/2025 umefanya Ziara ya kimafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara huku lengo kubwa likiwa ni kujifunza juu ya utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi mazao ghalani.
Ziara hiyo ambayo ni ya siku moja (1) imewahusisha Waheshimiwa Madiwani Kutoka Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Kondoa, Wataalamu, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huku naye mhe.Fatma Nyangasa ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa akiongoza msafara huo.
Amesema " sisi tumetoka Kondoa tumekuja Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kujifunza kwa vitendo namna mnavyoutekeleza mfumo wa uuzaji wa mazao ya kilimo yaani Stakabadhi ghalani, kwani sisi tumeanza lakini bado hatujafanya vizuri,kwaiyo tunaendelea kujifunza ili kuangalia zile changamoto ambazo tumepitia tulazifanyie kazi."....alisema Mkuu wa Wilaya ya Kondoa mhe.Fatma Nyangasa
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa