Halmashauri ya wilaya ya Masasi leo Tarehe 22/01/2021 imefanya semina elekezi kwa wenyeviti wa vijiji 166 katika kata 34 zilizopo ndani ya Halmashauri hiyo, kwa lengo la kuwajengea uwezo na weredi katika utendaji kazi wao pamoja na kukumbushwa juu ya matumizi mbalimbali ya sheria zinazoongoza vijiji
Hata hivyo mafunzo yalilenga pia kujadili taarifa mbalimbali za makusanyo ya fedha za ushuru na mapato mengine yanayokusanywa kupitia kwenye ngazi za vijiji ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kuchangia ukuaji wa mapato kwa ngazi ya kijiji na Halmashauri kwa ujumla.
Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri uliopo Masasi Mjini
Kaimu mkurugenzi bwana Lyoba Magabe kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Masasi Bi Changwa Mkwazu alisema” halmashauri imeamua kuandaa semina hii elekezi kwa wenyeviti wa vijiji ili kuwaleta karibu na wajiskie kuwa na wao ni sehemu ya menejimenti nan i watu muhimu katika kusimamia shughuli za maendeleo katika ngazi za vijiji, lakini pia kuwakumbusha katika kutekeleza wajibu na majukumu yao bila kuingilia ngazi nyingine za mamraka zilizopo kwenye kata zao”,
Bwana Magabe aliendelea kusema kuwa wengi wa wenye viti hao ni wapya hivyo baasi kupitia mafunzo haya yatawasaidia kutekeleza majukumu yao vema kwa weredi na kujiamini pia kuwezesha kutoa huduma nzuri kwa wananchi wanao waongoza,
Sambamba na hilo Mwenyekiti wa Halamshauri ya wilaya ya Masasi Mh. Ibrahimu Issa Chiputula ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mpeta alipokuwa akifungua mafunzo hayo alikuwa na hili la kusema “Nina mpongeza sana Mkurugenzi kwa kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo haya ambayo yatawasaidia sana wenye viti wa vijiji katika kutambua sheria na taratibu zinazoongoza, vijiji hivyo kurahisisha utendaji kazi wao”.
wenyeviti hao wa vijiji ameiyasa Halmashauri kupitia Mkurugenzi kuwa Mafunzo kama hayo ni muhimu sana kwao hivyo ameomba yawe yanafanyika mara kwa mara ili kuzidi kujengeana uwezo.
Wenye viti wa vijiji wakiwa wanafuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kutoka kwa wawezeshaji pamoja na ufafanuzi mbalimbali uliokuwa ukitotelewa na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya masasi siku hiyo ya semina elekezi.
Mratibu wa ICHF Bwana Peter Mushi akiwaeleza wenye viti wa vijiji kuungana na Halmashauri katika kuhimiza wananchi kujiunga na Bima ya Afya ichf iliyoboreshwa ambapo mwananchi anaweza kupata huduma za afya popote ndani ya Mkoa wa Mtwara kuanzia Zahanati, kituo cha afya, Hospitali za Wilaya na mkoa kwa shilingi 30,000/= kwa mwaka kwa idadi ya watu sita kwenye kaya moja.
Mratibu wa Tasaf ngazi ya Wilaya wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Bwana Thobias Mkude nae akitoa neno kwa wenye viti wa vijiji juu kuisaidia Halmashauri juu ya kuzitambua kaya masikini kweli kweli na kuacha tabia ya kuwapendekeza watu ambao wanajiweza, hata hivyo mratibu huyo aliwasihi wale wote ambao ni wanufaika na msaada huu wa tasaf kupitia kaya masikini kuhakikisha kuwa fedha wanayoipata wanaitumia vizuri kwa kubuni miradi mbalimbali ambayo itawaingizia kipato na hatimaye kuondokana na umasikini.
Mkuu wa Idara ya Mazingira Bi. Kulwa Maiga akitolea ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayohusu Mazingira mbele ya wenyeviti wa vijiji katika semina hiyo ya kuwajengea uwezo wenyeviti hao na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wananchi wanao waongoza katika vijiji vyao juu ya swala zima la utunzaji wa mazingira kwa ajili ya afya zetu na maendeleo yetu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa