WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe George Simba Chawene wamewasii wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na wajasiliamali wa mazao ya mifugo kote nchini kutumia teknologia zinazooneshwa katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi na kanda zingine ili kwa pamoja tuweze kuzalisha kwa tija mazao ya bidhaa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati kama kaulimbiu ya maonesho yaha inavyosema.
Mhe Simba Chawene aliyasema hayo wakati wa kufungua maonesho hayo ya Ki-taifa tarehe moja Agosti mwaka huu na kueleza kuwa wananchi wanaaswa kuzitumia Teknologia hizi ili waweze kuongeza uzalishaji kwani mkulima, mfugaji na mvuvi anapata fursa ya kufahamu njia bora na za kisasa za uzalishaji wenye tija katika eneo dogo au idadi ndogo ya mifugo.
“Nimetembelea mabanda nimejionea mazao yamestawi sana, ufugaji wa kisasa wa wanayama na samaki sasa teknologia hizo ziwafikie wananchi na sio kuishia katika maonesho haya kwani lengo ni kuwafikia wananchi ambao ndio wazalishaji wakuu wa mazao ya kilimo na mifugo mfano taasisi za majeshi zinafanya vizuri sana katika uzalishaji hivyo ni lazima wanachi wanaowazunguka wafundishwe kama watakataa wafundishwe kwa lazima” alisema Mhe. Simba Chawene.
Mhe Simba Chawene alisema kuwa, Sekta ya kilimo inachangia ajira kwa asilimia 65 na chakula kwa asilimia 100 huku katika pato la taifa sekta ya hii kwa mwaka 2015 ilichangia 29% na mwaka 2016 ilichangia kwa 29.1% hivyo ni sekta muhimu sana katika kuufikia uchumi wa kati unaoenda sambamba na uwepo wa viwanda.
Mhe Simba Chawene Ili kuboresha sekta ya kilimo serikali imekuwa ikisambaza mbegu bora na za mda mfupi pamoja na kutoka dawa za kupulizia mikorosho bure kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji na ubora wa zao la korosho kwa mia yote inayolima korosho ikiwemo mikoa ya lindi na mtwara.
Kwa upande wake Naibu wa waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha alisema kuwa ili kumkomboa mkulima, serikali imefuta Tozo na ada mbalimbali za mazao kwa mkulima lakini imepunguza ushuru kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3 kwa mazao ya biashara na asilimia 2 kwa mazao ya chakula ili wakulima wanufaike na kazi yao wanayoifanya, kusafirisha mazao chini ya tani moja hakuna kulipa ushuru.
Mhe Mhe. William Tate Ole Nasha alisema kuwa zao la korosho ndio zao linaloiliingizia nchi fedha za kigeni na ndio maana serikali imeamua kutoa dawa za kuulia wadudu bure na kusimamia uuzaji wa zao hilo kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao ni wa wazi na huru ili kuepuka uuzaji holela pamoja na kuzisafirisha kupitia bandari ya Mtwara na sio vinginevyo kwa korosha za Mtwara na Lindi.
Maonesho ya nanenane yalianza rasmi mwaka 1993 mjini mbeya na yanaendelea mpaka sasa ambapo kwa upande wa kanda ya kusini maonesho haya Kitaifa yalianza kufanyika mwaka 2014 na yamefanyika kwa mfululizo mpaka mwaka huu 2017 baada ya maonesho haya miaka mingine yataendelea kuadhimishwa kikanda.
Aidha, maadhimisho ya Ki-Kanda yatafanyika katika viwanja vya maonesho ya John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni - Dodoma; Nyahongolo – Mwanza; na Fatuma Mwassa - Tabora. Maandalizi na maonesho ya Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi wa mikoa husika. Washiriki wa maadhimisho ya Ki-Kanda wanatakiwa kuwasiliana na Sekretarieti za Mikoa husika ili kupata maelekezo na taratibu zingine za ushiriki.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa