Waziri MKuu wa Jamuhuri ya Muunganno wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amezindua jengo la wodi ya Wazazi katika kituo cha afya Chiwale lililogharimu shilingi milioni 138 738,460 lengo ikiwa ni kuboresha huduma za afya kwa akina mama na hivyo kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi.
Mhe. Waziri Mkuu amefanya Uzinduzi huo leo wakati wa ziara yake wilayani Masasi ambapo pamoja na Mambo mengine ametembelea kituo cha afya chiwale na kuzindua rasmi jengo hilo tayari kwa kuanza kutumika.
Mhe. Majariwa amewahakikishia wananchi kuwa serikali inataka kila kijiji kiwe na zahanati na kituo vya afya kwa kila Kata ili wananchi waweze kupata huduma zote za matibabu karibu na maeneo yao na sio kwenda mbali.
Kuhusu suala la dawa, Mhe. Majariwa amesema serikali inaendelea kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye kituo vyote vya kutolea Huduma za afya na mpaka kufikia mwezi desemba kila kituo kitakuwa na dawa za kutosha hivyo tatizo la kununua dawa kwenye maduka litaisha kabisa.
Pamoja na uzinduzi huo, mhe. Waziri Mkuu ameongea na watumishi wa wilaya ya Masasi ambapo amesisitiza uwajibikaji na uadilifu katika kusimamia matumizi ya fedha za serikali na kutekeleza majukumu yao ipasavyo, lakini pia amefanya mikutano ya Hadhara na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitolea ufafanuzi. Aidha kesho ataongea na wananchi Katika kata ya chiungutwa kabla ya kuendelea na ziara yake wilaya ya Newala.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa