Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganno wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwaamewata wakulima wa korosho wilayani masasi kupanda kupanda miche mipya ya korosho kama njia pekee ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo ndilo zao linalo waangizia kipato cha uhakika kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Mhe Kassim Majaliwa aliyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa kata ya Chiungutwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ikiwa ni ukamilishaji wa ziara yake ya kikazi wilayani Masasi na kueleza kuwa zao la korosho ni kati ya mazao yabiashara ambayo Serikali imeamua kuyasimami kwa karibu ikwa ni ni pamoja na kuhakikisha bei inapanda ili kuinua kipato cha wakulima.
Mhe Waziri Mkuu alisema “Serikali inatambua kuwa korosho ndio zao kuu la kiuchumi na inafanya jitihada kubwa kusimamia zao hilo, hivyo wananchi pandeni miche mipya ya mikorosho ya kisasa ili kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza kipato zaidi kwa mkulima”
Mfumo wa stakabadhi ghalani ndio mfumo ambao umewezesha wakulima kupata kuuza korosho kwa bei nzuri japo kuwa kuna changamoto ambazo zinasababishwa na viongozi wa vyama vya ushirika kwa kutokuwa waaminifu hali inayopelekea baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao zote.
Mhe Majaliwa alieleza kuwa kutokana na viongozi wengi wa Vyama vya ushirika kutokuwa waaminifu serikali imeendelea kuchukua hatua kwa viongozi hao ambapo kwa wilaya ya masasi jumla ya viongozi 56 wa vyama vya msingi waliosababisha baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao wamekamatwa na kuwekwa ndani kwa ajili ya hatua za kisheria.
Waziri Mkuu amewaeleza wakulima kuchagua viongozi waaminifu watakaosimamia vizuri fedha zao kwani kwa sasa serikali inaendelea kuchukua hatua kwa viongozi wa sasa waliosababisha baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao ambapo kwa msimu wa 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 1,241,294, 778 hazijalipwa.
Aidha Waziri Mkuu amemwagiza Mragisi wa Mkoa wa Mtwara kukigawa chama Kikuu cha Ushirika (MAMCU) ili kiweze kuhudumia wakulima kwa ufanisi zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo Chama hicho kinashindwa kuwasimamia wakulima ipasavyo kutokana na kuwa na eneo kubwa la usimamizi.
Ifahamike kuwa chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU kinasimamia wakulima wa Nanyumbu, Masasi na Mtwara hivyo imekuwa vigumu kufuatilia maslai ya wakulima ipasavyo.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa