Baadhi ya Wazazi na walezi wa kijiji cha Nantona, kata ya lipumbumbulu katika mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wanadaiwa kuwashinikiza watoto wao kufanya vibaya mitihani yao kumaliza elimu ya msingi ili wasichaguliwe kujiunga na kidato cha kwanza kwa kisingizio cha kuwa hawana fedha za kuwasomesha.
Hayo yalisemwa na wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Nantona wakati walipotembelewa na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi waliotembelea shule hiyo kwa ajili ya kuongea na wanafunzi hao changamoto zinazowakwamisha kimasomo na kuzitatua na hatimaye waweze kufaulu mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi na kujiunga na elimu ya sekondari.
Wanafunzi hao walisema kuwa pamoja na kutamani kufaulu vizuri mitihani yao wamekuwa wakikatishwa tamaa na wazazi au walezi wao kwa kuwaambia wajaze majibu ya uongo kwenye mitihani ili wafeli kwa kuwa hawana fedha za kuwapeleka sekondari,
Aidha wanafunzi hao walieleza kuwa pamoja na changamoto nyingi wanazokumbana nazo za kukosa muda wa kujisomea, ukosefu wa umeme lakini pia watoto wakike wanakumbana na changamoto ya kushinikizwa kuolewa mara baada ya kumaliza shule badala ya kuendelea na elimu ya sekondari.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo ndugu Beatus Jerome Mwakabilile alisema kuwa wazazina walezi wamekuwa chanzo kikubwa cha wanafunzi wa darasa la saba kutofanya vizuri mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa kuwatishia kuwapiga, kuwafukuza nyumbani na wengine kuwachinja.
Kutokana na changamoto hizo, Halmashauri pamoja na kuwapa ushauri lakini imeahidi kuwapa kipaumbele watoto watakaofaulu shule hiyo kwa kuwapeleka shule za bweni lakini pia kugharamia mahitaji ya kwenda sekondari ili kuwapa hamasa wanafunzi wa madarasa ya chini.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa