Jumla ya Wagonjwa 47 Kati yao Wanaume 22, Wanawake 25 wamefikishwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya kupata matibabu kutokana na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa kuharisha na kutapika ambao umegundulika kwenye kitongoji Cha Miesi, Kijiji Cha Mbangala Kata ya Lupaso halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Hata hivyo Kati ya Wagonjwa hao 47, Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 jumla ni ( 7) miaka 5 -15 jumla ni watano (5) miaka 15-49 wapo 32 na miaka 50- kuendelea ni Watatu (3).
Aidha taarifa inaeleza kuwa Wagonjwa wawili Me na Ke tayari wamepoteza maisha kutokana na uwepo wa mlipuko huo wa ugonjwa wa kuharisha na kutapika.
Akisoma taarifa katika kikao cha dharura kilichoitishwa na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Masasi mapema Leo June 18,2024 Afisa Afya na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bw.Said Ame amesema kuwa mnamo tarehe 10/06/2024 Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ilipokea taarifa kutoka kwa Mganga mfawidhi wa utimbe juu ya uwepo wa ugonjwa wa kuharisha na kutapika katika kijiji cha Mbangala, kitongoji Cha Miesi ambapo baada ya kupata taarifa hiyo timu ya dharura ya haraka (RRT) akiwemo na Afisa Afya mazingira, Daktari wa hospitali ya Halmashauri na mtaalamu Kutoka RUWASA walitembelea eneo la tukio katika Kijiji Cha Miesi na kuchukua sampo ya Maji yanayotumika (Mto Miesi) kwa ajili ya kufanyia vipimo vya Maabara.
Amesema pia tarehe 11/06/2024 katika kituo Cha Afya Chiungutwa walipokelewa Wagonjwa Watatu (3) wenye dalili za kuharisha na kutapika na hatmaye zikachukuliwa sampo kutoka kwa Wagonjwa na kupelekwa Maabara ya Ndanda kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya kimaabara na kubainika kuwa na vibrio cholerae.
Amesema kwa upande wa maiti iliyofariki kituo Cha Afya Chiungutwa ilifanyiwa vipimo vya haraka vya ugonjwa huo wa kuharisha na kutapika na kubainika uwepo wa vijidudu vya Vibrio cholerae.
Ameongeza pamoja na hayo kwamba zipo hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa Ili kudhibiti mlipuko huo ikiwemo kukutana na uongozi wa Kijiji na Kata kwa ajili ya kuelimisha na kuwakumbusha majukumu yao wakati wa mlipuko pamoja na kuwafahamisha uwepo wa Kambi ya matibabu ya Wagonjwa wa kuharisha na kutapika katika kitongoji Cha Miesi.
-Elimu juu ya Afya ya kujikinga dhidi ya Magonjwa ya mlipuko imetolewa kwenye mkutano wa Kijiji, maeneo yenye mkusanyiko,. maeneo huduma za vyakula na ngazi ya kaya katika Kijiji Cha Mbangala.
- Ugawaji wa vidonge 1580 vya water guard katika kaya 193 za Kijiji cha Miesi, kila kaya imepewa jumla ya vidonge viwili.
- Uhamasishaji wa Jamii juu ya ujenzi wa vyoo,ilani imetolewa kila kaya kuwa na choo ifikapo June 20/2014.
-Kwa kushirikiana na RUWASA kiasi Cha maji lita 20,000 kimesambazwa Kijijini Miesi.
-Kushiriki Shughuli za kutakasa maiti zote zilizohusishwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika ikiwemo na kusimamia maziko
-Kutembelea vituo vilivyopata Wagonjwa wa mlipuko kwa ajili ya kuelekeza na kuchukua tahadhari wakati wa mlipuko na taratibu zingine ikiwemo usambazaji na maelekezo ya matumizi ya dawa za utakasaji.
- Kufunga vilabu vya pombe za kienyeji kwa mujibu wa Sheria ndogo ya Afya na usafi wa mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
-Kuelimisha Wananchi umuhimu wa kunawa mikono Maji tiririka kutumia vibuyu chirizi na kutembelea kaya zilizopata Wagonjwa wa mlipuko kwa ajili ya kutakasa eneo na vyombo alivyotumia mgonjwa.
Hata hivyo katika kuhitimisha Taarifa yake Afisa Afya na Mazingira ameelezea baadhi ya changamoto ambazo zinazikabili hatua ambazo zimechukuliwa katika kupambana na mlipuko huo ni kwamba bado wapo baadhi ya Wagonjwa kutoka Miesi kuendelea kupata matibabu utimbe licha ya kuanzishwa Kambi Miesi, kuhama kwa wakazi kutoka Miesi kwenda Tandahimba hivyo kupelekea ugonjwa kusambaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya ulinzi na usalama ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.lauteri Kanoni pamoja na kumuagiza mkurugenzi aendelee Kutoa taarifa kwenye Vijiji na Kata zote juu ya uwepo wa mlipuko wa ugonjwa huo ili wananchi wapate taarifa na waweze kuchukua tahadhari namna ya kujikinga pia amelekeza uongozi wa Kijiji kuweka ulinzi getini ambao utahusika kuelekeza wanaotafuta matibabu utimbe kwanza waende kupata matibabu Kambini badala ya kwenda zahanati Moja kwa Moja
Pia ameendelea kuwasisitiza Wananchi wahakikishe ifikapo tarehe 20/6/2024 kila Nyumba inakuwa na choo bora na baada ya tarehe hiyo msako utafanyika wa vyoo kwa kila Nyumba.
Hata hivyo waliofariki ni Akili Issa Namwawa umri miaka 70 na Hadija Stamili Kitenge umri miaka 40.
Imeandaliwa na:
Winifrida Ndunguru
Afisa Habari MDC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa