Watumishi wapya 31 wa Idara ya afya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wamesisitizwa kutambua wajibu wao wa kuwahudumia wananchi vizuri kwani ndio lengo la serikali kuhakikisha wananchi wote wakiwemo wa vijijini wanapata huduma nzuri za afya katika maeneo yao kwa kuwaleta watumishi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Watumishi wapya na wawezeshaji wakimsikiliza mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi (hayupo kwenye picha)
Msisitizo huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu wakati akifungua semina elekezi kwa watumishi hao iliyolenga kuwajengea uwezo wa masuala mabalimbali ya utumishi wa umma pamoja na wajibu wao mkubwa katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Watumishi wapya wakisikiliza kwa makini maelekezo wakati wa mafunzo elekezi katika utumishi wa umma yaliytolewa na wataamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi
Mkwazu ameeleza kuwa Halmashauri inaupungufu wa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo afya, hivyo watumishi hao wapya watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma hali ambayo itapelekea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwani wataalamu wapo kwa kiasi Fulani.
“Vituo vyetu sasa vimepata wataalamu tuliokua tunawategemea, hivyo nategemea mabadiliko makubwa ya utoaji wa huduma unaozingatia maadili na taratibu za uuguzi kwa timu hii ya watu 31” alisema Mkwazu
Watumishi wapya wakifuatilia maelekezo
Mchango wenu unahitajika katika kuhakikisha wananchi hawalalamiki kwa kutokuhudumiwa vizuri kwani hali hiyo inasababisha wananchi kuvichukia vituo vya serikali na hatimaye kuamua kutumia dawa za kienyeji ambazo sio salama lakini pia sio lengo la serikali, alisisitiza Mkwazu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mheshimiwa Juma Satmah akitoa neno kwa watumishi wapya wakati wa semina elekezi (hawako pichani)
Mkwazu aliwaeleza kuwa “kazi ya kuhudumia afya za watu ni nyeti sana hivyo mnatakiwa kufanya kazi hii kwa moyo na kujitolea sana, wapokeeni vizuri nakuwa na lugha nzuri kwani ugonjwa hauna muda, mtu anaweza kuumwa muda wowote na lazima apate huduma, msichoke”
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa