Wakati jana tarehe 14.06.2017 watanzania wengi wakiadhimisha siku ya kuchangia damu duniani kwa kuchangia damu, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kupitia Idara ya Afya imefanya zoezi la kuhamasisha watumishi wa Halmashauri hiyo kuchangia damu kwa hiari ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha wananchi kuchangia damu.
Zoezi hilo ambalo lililenga watumishi wa Halmashauri hiyo kuchangia damu na kupata vipimo vya magojwa ya kisukari, moyo, Virusi vya Ukimwi na kupima uzito limefanyika leo katika Ofisi ya Halmashauri hiyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya serikali ya uchangiaji damu kwa hiyari kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wanaopoteza uhai kwa kukosa damu.
Akiongea wakati wa zoezi hilo Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dokta Charles Mkombe alisema kuwa mahitaji ya damu ni makubwa sana kwani damu inahitajika sana kuokoa miasha ya mtu wanaopata ajali, wakinamama wajawazito na wanapojifungu, wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji kwa hiyo damu ya kotosha ni muhimu sana kuwepo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkombe aliwashukuru watumishi waliojitolea kuchangia damu ambapo jumla ya chupa kumi (10) za damu zimepatika lakini pia watumishi wengi wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata ushauri kwani ili mtumishi aweze kufanya kazi vizuri ni lazima awe na afya njema.
Aidha dokta mkombe amesema kuwa mtu anayeweza kuchangia damu asiwe na uzito mdogo, asiwe na magonjwa kama kisukari, presha na maradhi mengine kwani kitendo cha kutoa damu kinaweza kumletea madhara kiafya.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa