Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka watumishi wa idara afya katika vituo vya kutolea huduma za afya kufanya kazi kwa weredi mkubwa ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto kabla na baada ya kujifungua kwa kuhakikisha zile sababu zinazopelekea vifo zinazuilika.
Dk kigwangalla ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya kutembelea vituo vya afya na zahanati katika Halamshauri ya Wilaya ya Masasi katika kituo cha Nagaga alipotembelea kituo hicho na kujionea vifaa tiba, vitendanishi na miundombinu ya kituo hicho na kueleza kuwa madaktari wana nafasi kubwa ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi kwa kuhakikisha wanapatiwa huduma bora kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Dk kigwangalla ameeleza kuwa azima ya serikali ni kupunguza vifo vya akina mama vinavyosababishwa kwa madaktari kutumia weredi wao ipasavyo katika kuwahudumia wamama wajawazito kabla na baada ya kufungua ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hawapati magonjwa ya kuambukizwa wakati wa kujifungua.
Akiwa kwenye kituo cha Nagaga Dk kigwangalla amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo bi Changwa M Mkwazu kuhakikisha anajenga chumba cha Upasuaji mdogo katika kituo cha Nagaga ili kusaidia kutatua matatizo madogomadogo ya upasuaji kwa wagonjwa watakaofikishwa hapo.
Pamoja na agizo la kujenga chumba cha maabara katika kituo cha afya Nagaga amesikitishwa na uwepo mashine ya kuhifadhi damu ambayo haijafanya kazi tangu ilipoletwa na wafadhili kutokana na ubovu wake kwani hazileti tija ya kutoa huduma bora
Kiutaratibu kila kituo cha afya kinapaswa kuwa na chumba cha upasuaji kikiwa na vifaa mbalimbali ikiwemo mashine za kutunzia damu ili mgonjwa anayehitaji damu baada ya upasuaji aweze kupata bila shida hivyo kutofanya kazi kwa vifaa hivyo kungesababisha vifo kwa wagonjwa ambao wanahitaji kuongezwa damu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla akiwa katika Zahanati ya lulindi, aliweza kukagua maeneo mbalimbali na kuwapongeza watumishi wa kituo hicho kwa kuweka mazingara safi pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi wa kijiji hicho hali inayowafanya wananchi wa kawaida kufurahia huduma.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa