Watendaji wa Vijiji na Kata wa Halamshauri ya Wilaya ya Masasi wametakiwa kuchapa kazi kwa kuboresha usimamizi wa shughuli zote katika maeneo yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi kwani wengi wao wanatekeleza kwa kasi ndogo sana hali ambayo inapelekea wananchi kulalamikia serikali kwa kukosa huduma.
Hayo ameyasema leo Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Jeremiah Lubeleje leo wakati akiwasilisha mada kuhusiana na Mwongozo wa fedha za LGCDG na Usimamizi wa miradi ya maendeleo tarehe 17.06.2017 wilayani masasi kwenye mafunzo ya watendaji kata na vijiji ya kuwajengea uwezo yaliyoendeshwa na Halmashauri hiyo baada ya kuona kuwa miradi mingi inayotekelezwa katika ngazi ya jamii haitekelezwa kwa wakati na kwa viwango stahiki.
“ni vema tubadilike tuwe watendaji wanaohudumia wananchi kwa kutumia nafasi zao vizuri ili kuwa na maendeleo katika maeneo yenu kwani serikali ya sasa inataka watumishi wafanye kazi kwa bidii akini pia kwa kazi kubwa” alisema Lubeleje.
Kuna baadhi ya vijiji Halmashauri imepeleka fedha za kutekeleza miradi tangu mwezi januari lakini mpaka saivi mradi haujaanza kutekelezwa, hali kama hii inaonesha mtendaji hutoshi kukaa kwenye nafasi hiyo maana moja ya majukumu yako ni kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na kwa kiwango kinachokubalika kama kuna watendai bado wako hivyo ni vema wabadilike haraka sana.
Lubeleje alisema, ruzuku ya Maendeleo isiyo na Masharti (LGCDG) ilianza mwaka 2004/2005 na ilisaidia sana kuziongezea Serikali za Mitaa uwezo katika utendaji kwa maeneo ya upangaji bajeti, usimamizi wa fedha na masuala ya manunuzi.
Alisema katika kipindi hicho, miradi mingi iliyotekelezwa katika sekta za afya, elimu, maji na kilimo lakini bado kulikuwa na changamoto za miradi mingi kuachwa viporo, vipaumbele vya nguvu za wananchi hazikuthaminiwa ipasavyo katika miradi hiyo na fedha zilizobajetiwa hazikuwa zinatolewa zote na kwa wakati na hivyo kusababisha kubaki na miradi mingi isiyotekelezwa.
Kwa sasa Serikali yetu ya awamu ya tano imefanya mapitio na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza hapo awali kwa kutumia Mwongozo wa mwaka 2016 wenye malengo makuu ya Ruzuku ya Maendeleo isiyo na Masharti (LGCDG) iliyoboreshwa yenye makusudu kuwa jamii inapata huduma bora na kwa wakati.
Afisa Mipango huyo aliwaeleza kuwa miradi inayotekelezwa na LGCDG inapaswa kuzingatia kutoa huduma kwa jamii, Vipaumbele vya jamii vinaainishwa ipasavyo, Juhudi za jamii zitambuliwe, ziwezeshwe na kuungwa mkono ili kuifanya serikali iweze kutoa huduma kwa jamii, Mgawanyo wa fedha ufanyike kwa usawa, kuboresha usimamizi wa fedha na maeneo yenye huduma duni yawe ni yenye kunufaika kutokana na ruzuku ya fedha za LGCDG.
Bwana Lubeleje alisema kuwa msisitizo wa matumizi ya fedha hizo ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa Miundombinu ya kilimo, maji safi na salama, elimu, afya, barabara na utawala bora kwa lengo la kutatua kero za wananchi wa ngazi ya chini.
Aidha aliwaeleza Watendaji wa Kata na Vijiji kuwa mtawanyo wa fedha za LGCDG uzingatie alimia themanini (80%) ya fedha hizo zitekeleze miradi ya maendeleo, asilimia kumi (10%) zielekezwe kwenye kujenga uwezo na asilimia kumi (10%) zitumike katika usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, “Tuchape Kazi, Tuache kufanya kazi kwa Mazoea”. Alisisitiza.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa