Watendaji wengi wa Kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wametakiwa kuendana na kauli mbiu ya serikali inayosisitiza kusimamia kwa hali na mali ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao kwani fedha hizo ndizo zinazotumika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Changwa M. Mohamed Mkwazu leo kwenye kikao cha mafunzo kwa watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri hiyo yaliyolenga kuwaelewesha kwa wale watendaji wanaokaimu na kuwakumbusha wale walioajiriwa majukumu yao ili waweze kufanya kazi kwa kuendana na kauli mbiu ya mheshimiwa Rais ya “HAPA KAZI TU kwa vitendo kwa kuhakikisha tunadhibiti upotevu wa mapato ambao kwa sasa ni upo kwa kiasi kikubwa sana.
Mkwazu amesema kuwa kuna baadhi ya watendaji wamekuwa na tabia ya kuacha wafanyabiashara wakitorosha mazao au kushirikiana nao kutoroja kwa kuwapa vibari vya kusafirisha mizigo hiyo kwa maslai yao, tabia ambayo inafanya halmashauri na vijiji vyetu kukosa mapato ambayo yangetumika kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao baada ya kukusanywa.
“ Tumeona tufanye mafunzo haya baada ya kuona baadhi ya watendaji hawajui kabisa cha kufanya kwa Halmashauri yao katika mambo tofauti ikiwemo usimamizi wa mapato na miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kwa fedha za serikali na inakuwa chini ya viwango” alisema Mkwazu.
Kwa sasa Halmashauri ipo kwenye msimu wa kuvuna na kuuza zao la choroko na utoroshaji umekuwa mkubwa mno wakati wakulima wapo kwenye vijiji na kata na watenndaji wapo na hawachukui hatua, “baada ya mafunzo haya ninategemea mtabooresha utendaji kazi wenu kwa kujua nafasi zenu katika kuleta maendeleo ya vijiji, kata na halmashauri kwa kutekeleza wajibu wanu vizuri kama ntakavyoelekezwa leo” alisema Mkwazu.
Mkwazu amewaambia watendaji hao kuwa , Halmashauri kila mwaka huwa inarejesha shilingi tano kwenye kila kilo ya zao la korosho kwa kila kijiji nia ikiwa ni kuhamasisha viongozi na wananchi ili waone umuhimu wa kulinda upotevu wa mapato ambayo hupotezwa na wananchi wasiouza korosh zao bia kufuata mfumo rasmi lakini cha kusiskitisha ni watendaji wachache sana ambao hutoa ushirikiano wa kutosha na wakati mwingine baadhi yao hudhubutu hata kutetea watu hao wanaoiibia halmashauri Ushuru.
Aidha kwa upande wake mtendaji wa kata ya Chiungutwa ndugu Joseph Kazibure amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka sana kwani yatatusaidia kuongeza uelewa kwa watendaji namna ya kufanya kazi zao za kila siku ikiwemo usimamizi wa miradi, ukusanyaji wa mapato pamoja na kutambua kanuni, taratibu na Miongozo ambayo mtumishi wa umma anatakiwa kufuata katika kutekeleza majuku yao.
Aidha Kazibure alikiri kuwa kwenye vijiji na kata kuna changamoto nyingi sana kwa ni kuna baadhi ya watendaji wanashindwa kusimamaia shughuli za maendeleo na wakati mwingine wao wanakuwa sehemu ya kikwazo cha maendeleo lakini kwa mafunzo haya “naamini kutakuwa na madadiliko makubwa katika kusimamia shughuli za maendeleo ikiwemo usimamizi wa mapato ambao ndio kiini cha utoaji wa huduma mbalimbali kwa umma ikiwemo ujenzi wa shule, vyoo, maradarasa na miradi mingine.
Naipongeza halamshauri kwa mafunzo haya kwani yataleta chachu kubwa katika kuboresha utendaji kazi kwa watendaji wa vijiji na kata lakini pia kuamusha ari ya kufanya kazi kwa wale wliokuwa wanazembea kwani wanjua serikali ipo na inawatazama na inawategemea katika kuleta maendeleo.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa