Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA) Wilayani masasi, imewaomba watendaji wa kata, vijiji na mitaa katika Halmashauri ya wilaya na mji Masasi kusaidia ukusanyaji wa kodi ya majengo katika maeneo yao ili kufanikisha ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia chanzo hicho.
Akizungumza katika kikao cha TRA na watendaji hao, Afisa mapato wa TRA Mkoa wa Mtwara Edwin Nkinga alisema, kodi ya majengo inatozwa kwa nyumba zilizopo katika maeneo yote yaani kuanzia ngazi ya vijiji, mitaa na kata ndio maana watendaji wanahusika moja kwa moja kutambua nyumba zote zilizopo katika maeneo yao ili zilipiwe kodi kama sheria inavyoelekeza .
Nkinga alieleza kuwa “Kikao hiki kinalenga kuwaelimisha nyinyi watendaji ili muweze kujua wajibu na majuku yenu katika ukusanyaji wa kodi za majengo ambapo majengo yanayotozwa kodi ni yale yanayotumika”
Nkinga alifafanua kuwa, Sheria ya kodi ya majengo inataja kiasi cha kodi kuwa ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida 20,000 kwa majengo ya ghorofa maeneo ya vijijini na 50,000 kwa majengo ya ghorofa maeneo ya mijini.
Aidha Nkinga alieleza kuwa baadhi ya majengo yanapata msamaha wa kodi yakiwemo majengo yanayotumiwa na Taasisi za Umma, majumba ya makumbusho au maktaba, majengo ndani ya makaburi, nyuma zilizoezekwa kwa nyasi na za udongo
Alisema watendaji hao wanatakiwa kusimamia ukusanyaji wa kodi za majengo katika maeneo yao kwa kutumia mfumo wa bili za majengo kutoka TRA kwa kutambua nyumba zote zilizopo kwenye maeneo yao kwa kujaza fomu kila mwaka ili kutambua idadi ya nyuma zilizopo na hatimaye ziweze kuliiwa kodi kulingana na hadhi ya jengo husika.
Kodi za majengo ni chanzo kingine cha mapato ya serikali, hivyo watendaji wote wanatakiwa kwa ajili ya nyumba zote zinazostahili kulipa kodi kwenye daftari la makazi katika maeneo yao.
Alisema sheria ya utoaji kodi ya majengo ya mwaka 1983 imeainisha maeneo yanayotozwa kodi ya majengo kuwa ni Halmashauri za miji, majiji, manspaa na wilaya.
Awali kodi za majengo ilikuwa inakusanywa na Halmashauri zote nchini, lakini mwaka 2016 kupitia bunge la bajeti serikali ilirekebisha sheria kodi ya majengo na kuipa TRA jukumu la kukadilia,kukusanya na kuhesabu kodi ya majengo katika halmashauri zote nchini.
Aidha, alisema kuwa kwa atakae kaidi kulipa kodi kwa wakti atachukuliwa hatua ikiwemo kulipa riba kama adhabu, kufikishwa mahakamani au kukamatiwa mali zake na kuuzwa ili kulipa kodi anayodaiwa.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa