Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata kwa majimbo ya ndanda na lulindi Halmashauri ya wilaya ya masasi mikoani mtwara wameptiwa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo na uelewa juu ya taratibu ,kanuni na sheria za uchaguzi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28, mwaka huu 2020.
Mafunzo hayo yametolewa leo tarehe 7 agosti, 2020 katika ukumbi wa jengo la zamani la halmashauri hiyo mjini masasi ambapo jumla ya wasimamizi 68 kutoka kata 34 wamepatiwa mafunzo hayo
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya masasi bibi Changwa Mkwazu amewakumbusha wasimamizi hao kuwa Tume ya uchaguzi imewaamini hivyo watekeleze majukumu hayo kwa weledi na uadilifu mkubwa wasifanye kazi kwa mazoea
"Tume ya uchaguzi imewateua ninyi kwa mujibu wa sheria , kanuni na uzoefu wenu katika masuala ya uchaguzi katika chaguzi zilizopita.
Mkwazu amewasisitiza Wasimamizi hao wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa majimbo ya Ndanda na Lulindi kuwa Pamoja na uzoefu walionao katika kuendesha chaguzi mbalimbali, wahakikishe wanazingatia maelekezo watakayopewa na Tume ya Uchaguzi na wasifanye kazi kwa mazoea, “ni lazima mtekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia Miongozo, sheria, Katiba na kanuni zinazosimamia zoezi la uchaguzi”
Aidha wasimamizi wasaidizi hao wamekula kiapo mbele ya Hakimu mkazi wa wilaya ya masasi mhe. Baptiste ikiwa ni sehemu ya kukiri kuwa watafanya kazi hiyo kwa Mujibu wa maelekezo waliyopewa kwenye Mafunzo hayo
Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 07/08/2020 mpaka tarehe 09/08/2020.
Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata kwa majimbo ya ndanda na lulindi wakila kiapo mbele ya Hakimu mkazi Mahakama ya Wilaya ya Masasi tarehe 07.08.2020
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa