Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omary Mgumba amezindua Siku maalumu ya ulaji na unywaji wa korosho leo tarehe 06.08.2020 katika maonesho ya Nanenane kanda ya kusini ikiwa ni njia ya kuujulisha umma juu ya uhumimu wa kula korosho lakini pia kuimarisha uchumi wa mkulima na Taifa kwa ujumla ikizingatiwa korosho inachangia zaidi ya TILIONI MOJA katika pato la taifa.
Katika uzindua huo wananchi walipata fursa ya kula korosho, kunywa juice na maziwa ya korosho, pombe (wine ) ya korosho pamoja na chapati, kashata, maandazi zilizotengenezwa kwa kutumia korosho ikiwa ni njia ya kuuhamasisha umma hususani wajasiliamali na walaji kuwa korosho inaweza kutumika kutengeneza vyakula na vinywaji mbalimbali ambapo kwa kufanya hivyo soko la korosho la ndani na nje ya nchi litakuwa la uhakika.
Mgumba amewataka wakulima wa korosho na wafanyabiashara wa korosho kujikita zaidi katika ubanguaji wa korosho ikiwa ni njia pekee ya kuiongezea thamani, kwani korosho iliyobanguliwa ina wigo mpana wa soko na ni rahisi kuhifadhika tofauti na korosho Ghafi , hii itasaidia kukabiliana na anguko la bei ambapo bei ya korosho imeendelea kushuka mara kwa mara.
Mgumba amesisitiza kuwa "Tujenge utamaduni wa kula bidhaa tunazozalisha ili kuimarisha soko la bidhaa zetu badala ya kutegemea soko la nje ambalo halina uhakika"
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa