Wananchi wa Wilayani Masasi Mkoani Mtwara mametakiwa kuzingatia usafi ikiwemo kuwa na vyoo bora, kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka chooni, kabla na baada ya kula pamoja na kuchemsha maji ya kunywa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuharisha kwani yanaweza kusababisha vifo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Said Mfaume baada ya wananchi 19 wa kitongoji cha chemichemi katika kijiji cha Namali kata ya Chikundi kukumbwa na ugonjwa wa huo na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambapo sababu kubwa imesemekana kuwa ni matumizi vya vyakula au vinywaji vilivyoambatana na vimelea vinavyoathiri tumbo.
Mfaume alisema kuwa uwepo kwa ugonjwa huo wa kuharisha na kutapika ikiambatana na maumivu ya tumbo, muungurumo wa tumbo na homa kwa baadhi ya wagonjwa, umewaathiri wagonjwa 20 wakiwepo watoto chini ya miaka mitano 3 na wenye umri wa miaka miano na kuendelea 17, kati yao wanaume 8 na wanawake 12.
Aidha Mfaume alieleza kuwa wananchi wa kijiji cha Namali hawana maji safi na salama ambapo wanapata maji kwenye visima vidogovidogo vilivyochimbwa kwa mkono katika mifereji/mabonde ya mto Chikudi na Mtunungu amabayo hata mifugo wanantumia
Ukosefu wa vyoo bora katika kijiji cha namali na kutozingatia usafi kwa kunawa mikono kwa sabuni na kuchemsha maji ya kunywa ni visababishi vikubwa vya maaradhi ya kuharisha katika kaya na jamii nyingi, hivyo wananchi wanapaswa kuzingatia usafi katika mazingira yote kwani madhara ya uchafu ni makubwa ikiwemo kusababisha vifo.
Mpaka sasa wagonjwa wote wananendelea vizuri.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa