Wananchi wa Kijiji na Kata ya Lupaso mekumbushwa kujenga mazoea ya kufanya usafi katika mazingira yao ikiwemo majumbani na maeneo ya wazi kila siku ili kuepuka magonjwa yanayosababishwa na uchafu katika maeneo yanayowazunguka na kwenye vyanzo vya maji.
Akiongea na wananchi hao baada ya kufanya usafi katika eneo la soko la kijiji, Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe Selemani Mzee aliwakumbusha wananchi kuhakikisha wanafanya usafi kwenye maeneo yao kila siku kwa kuhakikisha mazingira yana Kuwa safi lakini pia kutunza vyanzo vya maji kwa kuvihifadhi na kuacha tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo.
Selemani aliwakumbusha wananchi kuwa Ni vizuri kila mtu akawa na choo na kuwa na tabia ya kunawa mikono kwa sabuni kila wakati mara baada ya kushika kitu kichafu ili kuepukana maradhi kama kipindupindu ambayo ni gharama kubwa kuyatibu lakini pia yanasababisha vifo kwa haraka sana.
“ni lazima kila mwananchi ajue kuwa ana wajibu wa kuzua magojwa yanayosababishwa na uchafu kwa kufuata kanuni za usafi ikiwa ni pamoja na kusafisha mazingira, kuwa na choo, kunawa mikono kwa kutumia sabuni, kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji” alisisitiza Mkuu wa Wilaya
Aidha Mkuu wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kutunza chakula ambacho wanavuna ili kuepukana na tatizo la njaa ambalo mara nyingi linatokana na uuzaji holela wa mazao ya chakula
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa