• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 HALMASHAURI YA WILAYA MASASI

Posted on: December 7th, 2019

Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga  na Kidato cha Kwanza  mwaka 2020  kuwa ni  701,038 sawa na asilimia 92.27 ya wanafunzi 759,000 waliofaulu.

Akizungumza na waandishi  Jijini Dodoma Mhe. Jafo ameeleza kuwa wavulana waliochaguliwa ni 335,513 sawa na asilimia 47.86 na wasichana 365,525 sawa na asilimia 52.14.

Mhe. Jafo alifafanua kuwa kwa mwaka 2019 jumla ya wanafunzi 759,737 walifaulu sawa na asilimia 81.3 ya waliofanya mtihani, wakiwemo wavulana 363,999 sawa na asilimia 47.9 na wasichana 395,738 sawa na asilimia 52.08.

Kati ya waliofaulu wamo wanafunzi wenye Ulemavu 1,461 sawa na asilimia 0.19 wakiwemo wavulana 777 na wasichana 684 aliongeza Jafo.

“ Kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 3,145 sawa na asilimia 0.41 ya waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni, wanafunzi 970 watajiunga na shule za Wanafunzi wenye Ufaulu Mzuri zaidi; wanafunzi 1095 watajiunga na shule za Ufundi na wanafunzi 1,080 watajiunga na shule za bweni kawaida” alisema Jafo.

Aidha, wanafunzi 697,893 sawa na asilimia 99.59 wakiwemo  wavulana 361,866 na wasichana 395,692 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa katika kata mbalimbali nchini aliongeza Jafo.

Waziri Jafo aliongeza kuwa Mikoa 13 ya Dodoma, Geita, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora imeweza kuwachagua wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2019 katika shule za Sekondari za Serikali.

Aidha, jumla ya wanafunzi 58,699 sawa na asilimia 7.73 wakiwemo wavulana 28,567 sawa na asilimia 48.53 na wasichana 30,132 sawa na asilimia 51.33 ya waliofaulu, hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa alisema Jafo.

“Mikoa yenye uhaba wa vyumba vya madarasa na idadi ya wanafunzi waliobaki ni Arusha (4,739), Dar es salaam (5,808), Iringa (3,480), Kigoma (12,092), Lindi (1,695), Manyara (728), Mara (9,493), Mbeya (2,716), Pwani (2,918), Rukwa (686), Simiyu (6,616), Songwe (4,684) na Tanga (3,044)” alisema Jafo.

Jafo alibainisha kuwa Wanafunzi  waliobaki  watajiunga na kidato cha kwanza baada ya vyumba vya madarasa kukamilika.

“Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika shule za Sekondari.

Pia nawashukuru Walimu, Walimu Wakuu, Kamati za Shule, Maafisaelimu Kata, Wilaya na wa Mikoa pamoja na Viongozi wote wa Halmashauri na Mikoa na Wadau wa Elimu Nchini kwa kutoa ushirikiano katika kusimamia uendeshaji na utoaji wa Elimu bora Nchini.

Napenda kuwaasa wanafunzi wote waliochaguliwa kutumia fursa hii vizuri katika kujifunza” alisisitiza Jafo.

Wakati huo huo Mhe. Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ikiwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji shuleni ili kubaini changamoto mbalimbali na hatimaye ziweze kutatuliwa kwa haraka.

Ninaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya zilizobakiza wanafunzi kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ifikapo tarehe 29/02/2020 na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri husika kusimamia utekelezaji wa agizo hili ili kuhakikisha wanafunzi wote waliobaki wanajiunga na Kidato cha Kwanza ifikapo tarehe 02/03/2020.

Mhe. Jafo alimalizia kwa kutoa wito kwa Halmashauri na wadau wote wa elimu kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza Kidato cha Kwanza mwezi Januari mwaka 2020.

Mwisho.

kuangalia matokeo fungua hapo chini

.MTWARA_FORM_ONE_SELCTION_2020.pdf

MTWARA_FORM_ONE_SELCTION_2020...pdf





Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MSIGWA: MAAFISA HABARI NI SAUTI YA SERIKALI, TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MAENEO YENU.

    May 25, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU NA WAZALENDO ILI WANANCHI WAPATE HABARI SAHIHI NA KWA WAKATI.

    May 23, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa