MKuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewata walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani Masasi kuwa na Mipango madhubuti itakayo pandisha ufaulu wa elimu katika wilaya hiyo kwa mwaka 2018 kufuatia kutofanya vizuri katika matokeo ya mwaka 2017.
MKuu wa mkoa ameyasema Hayo Leo katika kikao kazi na walimu wote wa Wilaya ya Masasi katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Masasi ambapo amewataka walimu kujipanga katika kuboresha elimu kwa kuhakikisha ufaulu unapanda tofauti na sasa ambapo mkoa wa Mtwara umekuwa ukishika nafasi za mwisho mwisho katika matokeo ya darasa la saba, kidato cha pili na nne kwa miaka mitatu mfululizo.
“mimi ninaamini walimu mkiamua kupandisha ufaulu mnaweza, siri kubwa nkuweka mkakati wa pamoja wa namna ya kuhakikisha mitaala kwa madarasa ya mitihani yaani darasa la nne, la saba, kidato cha pili na cha nne ili waweze kupata muda wa kufanya mitihani y kujipima yenye hadhi ya kitaifa kabla ya mtihani wa Taifa” alisema Byakanwa.
Kuhusu changamoto ya mwamko mdogo wa elimu, mkuu wa mkoa amewashauri walimu kuwa na vibao vilivyoorodhesha majina ya wanafunzi waliowahi kufanya vizuri katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi taifa ili kuwapa ari watoto wengine ya kufaulu kama wenzao.
Aidha Byakanwa amewaeleza walimu na viongozi wa wilaya hiyo kuwa kwa shule itakayouwa ya mwisho kiwilaya katika matokeo ya mwaka huu 2018 itabidi mwalimu mkuu atoe maaelezo mbele ya mkuu wa mkoa kwa nini ameshika nafasi hiyo
Mkoa wa Mtwara umeshika nafasi ya 22 Kati ya mkoa 26 katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2017
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa