Wawezeshaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wapatiwa mafunzo kuhusu utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini( TASAF) kipindi cha pili awamu ya tatu namna ya kufanya uhakiki wa kaya 10315 za walengwa hao.
Uhakiki huo utahusisha kuondoa walengwa ambao hawana sifa za kuwepo kwenye mpango pamoja na kuingiza kaya Mpya ambazo hazikuwepo kwenye mpango ili zipate usaidizi wa kupitia TASAF kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umasikini
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bibi Elizabeth Mlaponi amewaasa wawezeshaji kuzingatia maelekezo watakayopewa ya namna ya kufanya uhakiki wa walengwa ili kuepuka kuweka walengwa hewa au wasiostahili kuwepo kwenye mpango.
Aidha Mlaponi Ameishukuru serikali kupitia TASAF kwa utekelezaji wa mpango huu unaolenga kusaidia walengwa kujikita kwenye shughuli za kukuza kipato na kujiimarisha kiuchumi ikiwemo ufugaji, kilimo, uvuvi na biashara ndogondogo ambapo baadhi ya walengwa wamefanikiwa kuboresha Makazi yao pamoja na kupata mahitaji muhimu.
Katika kipindi kwanza cha awamu ya tatu ya TASAF iliwafikia walengwa asilimia 70 ambapo takwimu zinaonesha umasikini wa mahitaji ya msingi kwa kaya umepungua kwa 10% na umasikini uliokithiri umepungua kwa 12% kwa kaya masikini sana nchini.
Katika kipindi pili cha awamu ya tatu ya TASAF kitafikia kaya 1,450,000 zenye jumla ya watu zaidi ya 7,000,000 kote nchini wanaoptatikana kwenye Halmashauri zote 185.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa