Wakulima wa mazao mbalimbali Wilayani Masasi Mkoani Mtwara wametahadharishwa kuacha tabia ya kuuza mazao yao kwa kutumia vipimo visivyohakikiwa ikiwemo matumizi ya kangomba wakati wa kuuza mazao yao kwasababu wanaibiwa bila kujua.
Tahadhari hiyo imetolewa na Kaimu meneja wakala wa vipimo Mkoa wa Mtwara ndugu David Makunga jana katika ziara ya kutoa elimu kwa wakulima namna ya kutambua mizani halali na batili wakati wanapouza mazao yao kwa wafanya biashara au kwenye vyama vya ushirika ili wasiibiwe.
Makunga alisema kuwa, wakulima wamekuwa wakiibiwa na wanunuzi kupitia mizani ambayo haina ubora au kangomba kwani vipimo hivyo havitoa kipimo halisi lengo ikiwa ni kujipatia faida kwa kuwaibia wakulima
Ili kuwatetea wakulima , wakala wa vipimo wanafanya ukaguzi na uhakiki wa mizani yote iliyopo kwenye vyama vya msingi kwa wilaya ya masasi na nanyumbu ili kubaini mizani mizima na mibovu na kutoa maelekezo ili wakulima wasiibiwe mazao yao na wanunuzi.
Katika zoezi hili kaimu meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa mtwara amesema kuwa katika ukaguzi hou mizani shahihi itawekwa alama maalumu ya stika (sticker) na chapa ili kumsaidia mkulima kutambua kama mzani anaotaka kupima mzao yake kama ni halali au batili.
“Ukaguzi na uhakiki huu wa mizani kwenye vyama vya msingi ni maandalizi ya msimu mpya wa ununuzi wa mazao mbalimbali ikiwemo choroko, ufuta, mbaazi na korosho ili kupunguza m
“katika msimu wa korosho kumetokea changamoto ya kutofautian n kwa tkwimu za ujazo wa korosho kutoka vyama vya msingi kwend chama kikuu hali iliyopelekea migogoro na kutoaminika kwa viongo kumbe kisa mizani inayotumika kupima inatofautiana” alifafanua Makunga.
Ili kumlinda mkulima serikali imeona itoe elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya vipimo lakini pia kutambua mizani halali inayotakiwa kutumika kupima mazao yao ili mkulima apate haki ya jasho lake, alisema Makunga
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa