Wajasiliamali wa mazao ya mifugo na kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wametakiwa kuwa na mtazamo wa kuzalisha mazao hayo kibiashara kwa kuzalisha kwa wingi na kuyaongezea thamani ili kukuza uchumi lakini pia kukuza ajira kwa vijana jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inalisistiza sana kupitia uchumi wa viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu (Aliyevaa nguo ya kitenge) wakati alipotembelea kikundi cha Umoja Farmers kilichopo kata ya Mpanyani kinachojishughulisha na ukamuaji wa mafuta ya alizeti
Hayo aliyazungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu wakati alipotembelea vikundi mbalimbali vya wajasiliamali vinavyojihusisha na ufugaji wa kuku na kilimo cha bustani katika kata za Namatutwe, lukuledi,ndanda na chikundi na kueleza kuwa ili wanavikundi waweze kujikwamua kiuchumi kwa vitendo lazima wazalishe kwa tija kwa kuangaia fursa zilizopo katika soko.
Mkwazu alieleza kuwa “ili kuendana na mahitaji ya soko uzalishaji lazima uwe wenye tija, natarajia kuona kikundi kinakuwa na kuku kuanzia 500 hapo unaweza kuona kweli wanakikundi wanaweza kuongeza kipato kupitia mradi huu sio kuku 40 wanaikundi 10 huo sio ujasiliamali ninaoutaka mimi”
Wanakikundi wa kata ya Namatutwe wanaojihusisha na ufugaji wa kuku na wadau wa maendeleo wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu wakati alipotembelea kikundi hicho
Kikundi kinapopata mkopo Halmashauri lazima utumike kwenye mradi uliokususdiwa na sio kuanza kufanya biashara zingine tofauti na mradi ulioombewa mkopo, hii inasababisha kikundi kutokuwa na miradi ambayo ina tija na hivyo kutofikia malengo ya serikali ya kukuza uchumi kwa wanavikundi ambao ni akina mama na vijana kupitia ujasiliamali.
Mkwazu ameeleza kuwa, baadhi ya wanavikundi wanafanya ujasiliamali wa kizamani yaani malengo yao hayalengi kutumia njia za kisasa kama njia kuu ya kuzalisha kwa wingi na ubora unaoendana na mahitaji ya soko ili kukuza uchumi wa wanakikundi, ni vema sasa mbadilike tumieni wataalamu waliopo kupata ushauri laini pia muwe na mitazamo ya mbali ikiwemo kuzalisha kwa wingi na kuanzisha kiwanda kulingana na malighafi mnayozalisha.
Mafuta ya alizeti yanayotengenezwa na kikundi cha Umoja Farmers kilichopo Kata ya Mapanyani
Kwa upande wa miradi ya jamii ambayo vimewezeshwa miundombinu hususani ya mashine za kukamulia mafuta na mhogo Mkwazu amewakumbusha kuwa ni vema wakatunza miundombinu hiyo kwa kuifanyia matengenezo ili iendelee kutumika lakini pia kufikia hatua kununua malighafi kwa wananchi ili wananchi waweze kunufaika na mradi badala ya kusubiri serikali kuwafanyia kila kitu.
Kikundi cha Liputu kinachojihusha na kilimo cha bustani kinachotumia umwagiliaji wa matone kata ya Ndanda
Aidha Mkurugenzi amelishukuru shirika la Agha khan kwa ushirikiano wanaofanya katika kusaidia vikundi vya ufugaji na kilimo kwa kutoa elimu ya masoko na uzalishaji kibiashara ambapo elimu ya kutumia pembejeo ya kilimo na mifugo ikiwemo mbegu bora na madawa ya kuzuia magonjwa inatolewa kwa wajasiliamali hao na matunda yanaonekana.
Afisa ugani wa Kata ya Namatutwe Silaji Magambo akitoa maelezo ya kikundi cha ufugaji kuku wakati wa ziara ya kutembelea viundi hivyo
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa