Wajasiliamali wenye ujuzi wa kubangua korosho wilayani Masasi watafaidika na fursa ya ubangua korosho zilizonunuliwa na serikali lengo ikiwa in kuziongezea thamani lakini pia kuwaogezea kipato wajasiliamali hao.
Hayo yalizungumzwa na Kaimu Naibu katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Rudovick James Nduhiye alipotembelea wilayani hapo jana na kueleza kuwa, lengo la kikao hicho ni kuwaeleza wajasiliamali wenye elimu ya kubangua korosho ili waweze kunufaika na ujuzi kwa kuwawekea utaratibu wa kushiriki ubanguaji wa korosho zilizonunuliwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kaimu Naibu katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Rudovick James Nduhiye (wa katikati) akiwa kwenye kikao na wajasiliamali Wilayani Masasi kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bibi Neema Joseph na wa kwanza kulia ni Afisa kilimo Wa Halmashauri hiyo bwana Tamba Winfrid
Nduhiye alieleza kuwa wajasiliamali watakao shiriki ubanguaji wa korosho watalipwa shilingi 1000 kwa kila kilo ya korosho iliyobanguliwa, kuhusu upatikanaji wa korosho hizo serikali itapeleka katika maeneo yote yaliyochaguliwa kwa ajili ya ubanguaji wakiwa wamepata mikataba ya kufanya kazi hiyo.
Wajasiliamali wakiwa kwenye kikao
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina viwanda 6 vya kubangua korosho ambavyo vinasimamiwa na vikundi vya wajasiliamali, ambapo kwa mujibu wa Nduhiye ameeleza kuwa viwanda hivyo vitatumika kubangulia korosho baada ya wataalamu kuvikagua ambapo hadi kufikia tarehe 15 machi, 2019 viwanda vyote vitatakiwa kuwa vinafanya kazi.
“ Serikali imeamua kubangua korosho kwa kushirikisha wajasiliamali kama sehemu ya kutambua mchango wao na kuwaongezea kipato kupitia ujuzi wao” alisema Nduhiye.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Neema Joseph amesihii wajasiliamali wote ambao wanaujuzi wa kubangua korosho wajitokeze kwa wingi kwani ni fursa nzuri ya kujikwamua kiuchumi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa