Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu,Lyoba Makabe kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi. Changwa Mkwazu amezindua mafunzo maalumu ya siku mbili kwa ajili ya kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani ikiwa ni pamoja na kujifunza zaidi kuhusu kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza Halmashauri lengo ni kuepuka mgongano wa kikanuni kupitia vikao na mabaraza kati ya waheshimiwa madiwani na halmashauri ,
Aidha kupitia mafunzo hayo aliwaasa waheshimiwa madiwani kuwa makini kwa kuyafuatilia mafunzo hayo kwa kina ili yaweze kuwaletea tija na ufahamu katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Aidha Bi. ambaye ndiye mgeni rasmi katika mafunzo hayo ambayo yalifanyika kwa muda wa siku mbili, wakati wa kufunga mafunzo hayo alisema' Naipongeza halmashauri ya wilaya ya masasi kupitia mkurugenzi kwa kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo haya kwa waheshimiwa madiwani ambayo yaliendeshwa na wakufunzi kutoka chuo cha serikali za mitaa Homboro kilichopo Dodoma na kuwaomba waheshimiwa madiwani kuzingatia na kuzisoma kanuni mbalimbali na miongozo inayoongoza halmashauri ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi
Aliendelea kumpongeza mkurugenzi kwa kuwapatia simu maarufu kama vishikwambi waheshimiwa madiwani wote pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ili simu hizo ziweze kuwasaidia kwenye kazi zao hasa kwenye vikao na mabaraza ambapo jumla ya vishikwambi sabini vilitolewa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni sitini na nane lengo likiwa ni kupunguza garama za matumizi ya uchapishaji na utoaji nakala wa taarifa mbalimbali kwa ajili ya vikao lakini pia kuendana na zama za matumizi ya sayansi na teknologia.
Waheshimiwa madiwani na vishikwambi vyao wakiwa wanafuatilia kwa ukaribu mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kutoka kwa wakufunzi wao.Afisa tehema wa Halmashauri ya wilaya ya masasi bwana anorld marandu akiwapa semina elekezi waheshimiwa madiwani juu ya matumizi sahihi ya vishikwambi walivyopatiwa .
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa