Biashara ya mazao ya misitu ikiwemo Mkaa, kuni, mbao na mengine wilayani Masasi imekuwa na changamoto kutokana na wengi wao kutofuata sheria na kanuni ya misitu ikiwemo kutokuwa na vibali na leseni za kufanya biashara hiyo.
Kutokana na changamoto hiyo Wakala wa Misitu Wilayani Masasi inawakumbusha wafanyabiashara wote kutambua sheria na kanuni zilizowekwa na idara hiyo ili waweze kutambulika lakini pia kuzuia uvunaji holela wa mazao Hayo hali inayopelekea uharibifu mkubwa wa misitu.
Akiongea na wananchi wakati wa ziara ya kutoa elimu juu ya sheria zinazotakiwa kufuatwa, Afisa misitu mbwana Milanzi alisema kuwa idara ya misitu inapita kutoa elimu juu ya sheria na taratibu za kufanya biashara ya misitu kwa mara ya mwisho na baada ya Elimu hii sheria itafuata mkondo wake.
"Sio mara ya Kwanza kwa wakala wa misitu wilani Masasi kutoa elimu hii kwa wananchi, hivyo watu wanafahamu ndio maana wakikutana na watu wa maliasili wanakimbia. Hivyo kwa anayetaka kuendelea kufanya biashara ya misitu ni lazima afuate sheria ili kulipa kodi ya serikali na kulinda misitu yetu ambayo ina faida kubwa kwa maisha ya binadamu" alisema milanzi.
Sheria hizo ni :
1. Kila mfanyabiashara lazima asajiriwe na wakala wa huduma za misitu tanzania
2. Kila mvunaji wa mazao ya misitu lazima awe na leseni na kila gunia la mkaa linatakiwa kukatiwa risiti
halali ya malipo ya serikali kuu na Halmashauri.
3.kila msafirishaji wa mazao ya misitu lazima awe na kibali kusafirishia kianachomruhusu kusafirishia
mazao Hayo ikionyesha Mahali mazao yanapotoka na yanapoenda ikiambatanishwa na leseni
4. Usafirishajk wa mazao ya misitu ni kuanzia saa 12.00 asubuhi hadi 12.00 jioni.
5. Ni marufukukusafirishia mkaa kwa kutumia baiskeli au pikipiki
6. Biashara ya mkaa lazima ifanyinyike katika maeneo maalumu yaliyoainishwa.
7. Ni marufuku kwa mfanyabiashara wa mkaa kufanya biashara hiyo kandokando ya Barabara au
nyumbani
8. Kwa wanunuzi wote wa mkaa kwa ajili ya matumizi ya kaya lazima awe na risiti halali ya serikali
inayoonesha malipo halali ya serikali inayoonesha malipo halali yaliyofanyika kwa idadi ya magunia ya
mkaa aliyonunua.
NB: Gharama ya usajili ni shilingi 261,000 kwa mwaka, kila gunia gunia la mkaa litalipiwa shilingi 2650 kama sheria 2 inavyoainisha
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa