Halmashauri ya wilaya ya Masasi leo tarehe 04/02/2021 imefanya kongamano kubwa ambalo limekutanisha wadau mbalimbali wa Elimu wanaopatikana ndani ya Halmashauri hiyo kwa lengo la kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya Elimu ndani ya Halmashauri hiyo,
Akifungua kongamano hilo Mh. Ibrahimu Chiputula ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa kata ya Mpeta ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa na haya ya kusema kwa wajumbe 'NIkiwa kama mwenyeki wa Halmashauri nililazimika kukaa na maafisa elimu wote pamoja na Mkurugenzi na kuandaa kongamano hili ili kuwaleta wadau wote pamoja na kujadili changamoto hizi kwa pamoja na kutafuta namna ya kuzipatia ufumbuzi wa kina na hatimae Halmashauri yetu iweze kusonga mbele katika sekta ya Elimu,
katika mjadala huo changamoto mbalimbali ziliweza kujadiliwa ikiwemo changamoto ya baazi ya wazazi kuwakata watoto wao wasifanye vizuri katika mitihani yao ya mwisho ili wasifaulu kwa kisingizio cha kukosa uwezo wa kusomesha watoto wao, lakini pia kuna changamoto ya wazazi kwenda mpaka mashuleni kuwasubiri watoto wao nje siku ya mitihani ya taifa kwa lengo la kuwafanyia sherehe kitendo ambacho kinamfanya mwanafunzi asifanye vizuri kwa kuwazia sherehe anapokuwa kwenye chumba cha mtihani, wazazi kushindwa kuchangia chakula kwa watoto wao, kukosekana kwa ushirikiano wa kutosha kati ya wazazi, jamii na shule, lakini pia upungufu mkubwa wa walimu hasa wa masomo ya sayansi.
Mwisho wa kongamano hilo wadau hao waliondoka na maazimio mbalimbali yaliotokana na changamoto hizo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika sekta hiyo ya Elimu ndani ya Halmashauri ya wilaya ya masasi.
Afisa Elimu Msingi Bi. Elizabeth Mlaponi ambaye pia alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi akichangia na kufafanua baazi ya hoja zilizoibuka katika mjadala mkali uliokuwa ukiendelea wakati wa kongamano hilo (wa kwanza kwenye picha)
Afisa Elimu Sekondari Ndugu.Ally Nyambate nae akitoa mchango wake mbele ya wadau wa Elimu juu ya changamoto mbalimbali zinzoikabili secta ya Elimu na namna ya kuzitafutia ufumbuzi ili Halmashauri ya wilaya ya Masasi iweze kusonga mbele.
Afisa Taaluma wa Halamshauri ya wilya ya Masasi Ndugu, Rajabu akitoa taarifa ya Elimu Msingi kwa niaba ya Afisa Elimu Bi. Elizabeth Mlaponi wakati wa kongamano la wadau wa Elimu lililofanyika leo kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za Elimu zinazoikabili Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.
kwa taarifa zaidi juu ya ripoti hiyo kwa Idara ya Elimu Msingi pakuwa kablasha hili hapa..RIPOTI YA ELIMU MSINGI.doc
Afisa Takwimu na Vifaa wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Ndugu.Shabani Kinyongo akitoa ripoti ya Elimu sekondari kwa niaba ya Afisa Elimu katika kongamano la wadau wa Elimu lililofanyika Mbuyuni katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi la kujadili changamoto za Elimu..
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina jumla ya shule za sekondari 29. Kati ya hizo shule 27ni za serikali na shule2 ni za binafsi. Shule 23 zina wanafunzi wa kidato cha Kwanza mpaka cha Nne, shule 4 zina wanafunzi wa kidato cha Kwanza mpaka kidato cha tano, shule1 ina kidato cha tano na sita.
Kwa taarifa zaidi kwa Elimu sekondari angalia kablasha hili.... RIPOTI YA ELIMU SEKONDARI.doc
Mgeni rasmi Mh. Ibrahimu Issa Chiputula pamoja na wadau wengine Meza kuu wakitoa zawadi za vyeti Maalumu na pesa taslimu kwa shule mbalimbali zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya upimaji wa Darasa la Nne pamoja na Mitihani ya Taifa ya kumaliza Elimu ya Msingi kwa Mwaka 2019/2020 ambapo matokeo ya shule hizo ilikuwa kama ifuatavyo
5 .1. Shule 10 bora:
5.1.1 Jedwali Na.9: (a) linaonesha shule 10 zenye ufaulu mzuri Kihalmashauri
NA. |
JINA LA SHULE |
WALIOFANYA MTIHANI |
WALIOFAULU |
NAFASI YA WILAYA (122) |
NAFASI KIMKOA (630) |
NAFASI KITAIFA |
WASTANI WA UFAULU (250) |
|
||||
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
|
||||||
|
||||||||||||
1 |
Mkalapa |
19 |
22 |
41 |
19 |
22 |
41 |
1 |
2 |
367 |
198.36 |
|
2 |
Mtakuja I |
9 |
6 |
15 |
9 |
6 |
15 |
2 |
13 |
1077 |
172.06 |
|
3 |
Luagala |
10 |
11 |
21 |
9 |
11 |
20 |
3 |
19 |
1190 |
170.04 |
|
4 |
Ndwika Mazoezi |
18 |
30 |
48 |
17 |
30 |
47 |
4 |
20 |
1327 |
166.02 |
|
5 |
Lusonje |
9 |
13 |
22 |
9 |
10 |
19 |
5 |
35 |
1542 |
161.31 |
|
6 |
Liputu |
11 |
18 |
29 |
10 |
18 |
28 |
6 |
40 |
1743 |
157.34 |
|
7 |
Mkang'u |
22 |
29 |
51 |
20 |
27 |
47 |
7 |
39 |
2047 |
155.62 |
|
8 |
Nangoo |
25 |
54 |
79 |
25 |
54 |
79 |
8 |
47 |
2248 |
153.37 |
|
9 |
Mkachima |
14 |
11 |
25 |
13 |
11 |
24 |
9 |
53 |
2027 |
152 |
|
10 |
Manyuli |
14 |
16 |
30 |
12 |
16 |
28 |
10 |
56 |
2073 |
151.2 |
|
NB: Halmashauri ya Wilaya Masasi ina jumla ya shule za Msingi 131, kati ya hizo shule zilizofanya mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi ni 124. |
|
Wadau mbalimbali wa Elimu wakiwa kwenye Mkusanyiko wa pamoja wakati wa kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu na kujadili njia mbalimbali zitakazowezesha kutatua changamoto hizo na hatimaye kuinua kiwango cha Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa