Mwenge wa uhuru kitaifa 2024 umetembelea na kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa katika shule ya msingi Mwena iliyopo kata ya Mwena, jimbo la Ndanda Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizokuwa na miundo mbinu michache ikilinganishwa na idadi ya Wanafunzi waliopo, ambapo kabla ya utekelezaji wa mradi huu shule ilikuwa na vyumba vya madarasa 10 hali iliyosababisha mlundikano mkubwa wa Wanafunzi madarasani .
Kwa mujibu wa taarifa ya mradi huo unaeleza kwamba, mnamo tarehe 24/04/2023 shule ilipokea kiasi cha fedha shilingi 120,000,000,00 kupitia mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa pamoja na utengenezaji wa samani (madawati 15, meza na kiti cha mwalimu kwa kila darasa )
Aidha pamoja na ujenzi wa mradi huo kuanza rasmi tarehe 18/05/2023 kupitia "Force Account" na ulikamilika tarehe tarehe 10/08/2023 kwa asilimia 100 ambapo vyumba vitano (5) vya madarasa na ofisi 2 za walimu zimejengwa. Pamoja na utengenezaji wa madawati 75,viti 5 na meza 5 za walimu.
Mchango wa jamii katika mradi huo ni kiasi cha shilingi milioni mbili na laki nne (2,400,000/=) ambapo walifanya kazi za kuchimba msingi, kujaza kifusi, kuchota maji na kusomba tofali, ambapo kutokana na mchango huo wa jamii wameweza kujenga ofisi 2 na kujenga sehemu ya kunawia mikono .
Hata hivyo mradi huu tayari ulianza kutumika tarehe 16/10/2023 na umesaidia kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati na kuwezesha wanafunzi ,kusoma vizuri wakiwa wamekaa kwenye madawati.
Shule ya msingi Mwena ina jumla ya Wanafunzi 1,053 wakiwemo Wavulana 529 na Wasichana 524, mahitaji ya walimu ni 22 waliopo 10, na mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 22 vilivyopo 15 hivyo shule ina upungufu wa vyumba 7vya madarasa.
Kazi iendelee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa