Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara Ndg. Yusuph Nannila ambaye aliongozana na Viongozi mbalimbali wa Kamati ya CCM Mkoa akiwemo Ndg. Alhaj Saad S. Kusilawe (Katibu CCM Mkoa), Lucas M. Milasi (MNEC Taifa) pamoja na Viongozi wa CCM Wilaya ya Masasi wakiwa kwenye picha ya pamoja walipokuwa wakikagua na kupokea Taarifa ya Miradi Mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya Masasi ukiwemo ujenzi wa Hospitali ya Wilaya katika kata ya Mbuyuni, Ujenzi wa Kituo cha Afya katika kata ya Chiungutwa, Ujenzi wa stendi ya mabasi Ndanda Pamoja na ujenzi wa vyumba Viwili vya Madarasa na Chumba kimoja cha ofisi ya Walimu katika Shule ya Msingi Chikundi,amesema kuwa miradi hii itachochea maendeleo si kwa wana Masasi pekee bali na Tanzania kwa ujumla.
Huu ni mradi wa stendi ya mabasi Ndanda ambao unatekelezwa kwa Fedha zinazotokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri, Mradi unategewa kugharimu kiasi cha shilingi 117,147,028.40/ katika awamu ya kwanza lengo la mradi utakapokamilika ni kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi kwa serikali kuu, Mradi unategemewa kuwa na Vibanda zaidi ya 120 vya Biashara Pamoja na kibanda cha kutoza ushuru.
Wananchi na wanachama wa CCM nao hawakuwa nyuma walijitokeza kwa wingi katika eneo la tukio ili kushuhudia Viongozi hao wa Mkoa walipotembelea eneo la Mradi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa