• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATIWA MAFUNZO KUELEKEA UPOKEAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI

Posted on: January 6th, 2025

Vikundi 28 vya Wanawake Vijana na watu wenye ulemavu vinavyotarajia kupata mkopo wa  asilimia 10% kutoka  Halmashauri ya Wilaya Masasi Leo Tarehe 06/01/2025 vimepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya matumizi sahihi ya fedha watakazopatiwa hivi karibuni ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa na serikali.


Vikundi hivyo vya  Wanawake ni 15 na Vijana ni 13 huku kundi maalumu la watu wenye ulemavu hakuna waliojitokeza.

Pamoja na kufundishwa  matumizi sahihi ya fedha, Lakini pia wamefundishwa juu ya utawala na Uongozi bora, Elimu juu ya kuzuia na kupambana na rushwa , Usimamizi wa miradi, uendeshaji, ufuatiliaji na usimamizi wa miradi pamoja na ujazaji wa mikataba.


Bw. Shida Chihongaki ni Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Masasi naye ni miongoni mwa walioshiriki katika kuviwezesha kielimu Vikundi hivyo kwenye mafunzo hayo ambapo amesema kwamba jukumu lao la msingi ni kuzuia, kupambana na rushwa "tunazuia kwa Kutoa elimu, tunapambana kwa kumkamata yule ambaye amekiuka miongozo na ndio maana wenzetu wa Halmashauri hapa wametuita sisi katika mafunzo yenu haya tumekuja kuzungumza mapema kabla ya tukio halijatokea, maana tumeambiwa mlianza kwa kuomba, mkaandika maandiko ambayo yamepita katika sehemu mbalimbali ikwemo hata kwetu TAKUKURU yalikuja pia tukayafanyia kazi, na hatmaye vikundi 28 vimepita katika Mchakato na hatmaye leo hii mpo hapa, na ndio maana leo hii sijamtuma mwakilishi nimekuja mwenyewe kuwapa elimu hii kwaiyo lengo letu ni kuhakikisha kwamba fedha hizi ambazo zinatolewa na serikali zinatumika kama ilivyokusudiwa"..alisema Chihongaki....

Amesema Vikundi hivyo pia vinapaswa kufahamu yale majukumu matatu ya Msingi ya TAKUKURU ikwemo kuchunguza vitendo vya rushwa ambapo baadaye ikafanyiwa maboresho na kuwepo jukumu la Kutoa elimu Kwa umma Kama ambavyo wamefanya hapo, jukumu lingine ni kufanya utafiti kubaini mianya ya rushwa, ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Serikali kwasababu hiyo mikopo wanayopewa ni fedha za Serikali na zina makusudi maalumu.

" Wakati tunafanya mchakato wa kupata hivi Vikundi sisi tulikuwa tunapita kuvikagua hivi Vikundi kimoja baada ya kingine ambavyo vinasemekana vinataka mikopo na pia vikundi vya miaka ya nyuma lakini yapo baadhi ya maeneo tumepita na kubaini vikundi hivyo havipo Kabisa (hewa ) yaani watu wamekaa wameandika andiko huku wakisubiria fedha ikitoka wagawane sasa nawashauri fedha ambazo mnaenda kuzipata nendeni mkazifanyie kazi Kama maandiko yenu mlivyoandika ili zoezi lilete tija, na ninahaidi baada hizi fedha Kutoka sisi tutapita kukagua kila kikundi kuhakikisha vinafanya kazi na malengo ya Serikali yanatimia ya kuwainua akina mama, Vijana na watu wenye ulemavu, kwaiyo msiende kufanya tofauti naomba viongozi hakikisheni mnalisimamia hilo na mshirikiane "

Aidha Kamanda Chihongaki akahitimisha kwa kuwaomba wanavikundi hao kuendelea Kutoa ushirikiano kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao kama ilivyokusudiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo imetolewa " Sasa kwenye miradi hapa tusaidiane, miradi ipo kwenu kwenye maeneo yenu, ni yenu hiyo mkiona inakwenda kinyume na utaratibu mtuambie" alisisitiza

Hata hivyo ifahamike kuwa kiasi cha fedha kitakachokopeshwa kwenye Vikundi hivyo 28 kitapatikana baada ya vikundi kuridhia kuwa tayari kupokea na kufanyia kazi fedha waliyoidhinishiwa.


06/01/2025

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa