Wajumbe wa kamati ya Elimu, Afya na Maji ya Halmashauri ya wilaya ya Masasi wakiwa kwenye Mkutano maalumu unaolenga kutambulisha mradi, wa Uhamasishaji wa Huduma za uzazi wa Mpango katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi . Lengo la mradi huu ni kuboresha huduma za uzazi wa Mpango, na huduma kwa watu waliopatwa na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kwa kutumia njia ya uzazi wa Mpango ya muda Mrefu
Utafiti unaonyesha kuwa kati wanawake 100, 000 wanawake 556 wako kwenye hatari ya kufa kutokana na uzazi hii ni sawa na wanawake 24 hufa kila siku kutokana na Matatizo ya uzazi.
Kwa mkoa wa Mtwara kwa miaka mitatu(2014_2016) idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi ni 200,. Kwa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Vifo 33 vilitokana na uzazi kwa kipindi cha miaka 3
Tafiti zinaonesha kuwa kama Uzazi wa Mpango utazingatiwa vifo vitokanavyo na uzazi vitapungua kwa 43.4%
Kwa Halmashauri ya wilaya ya Masasi, inakadiliwa wanawake 6 Kati ya 10 walioko katika lika ya uzazi (15_49) huzaa, hii inapelekea ongezeko la watu kuwa 2.1 kwa halmashauri ya wilaya ya Masasi wakati ongezeko la watu Kitaifa ni 2.7 hii inaonesha matumizi ya uzazi wa Mpango ni kidogo
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa