Tatizo la umeme katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vilivyopo maeneo ambayo hayana umeme na nyumba za watumishi wa idara ya afya katika Halmashauri ya wilaya na Mji Masasi litakuwa historia baada ya Halmashauri hizo kwa kushirikian na halmashauri rafiki ya Enzkreis ya nchini ujerumani kuweka umeme jua katika vituo hivyo lengo ikiwa ni kuboresha utoaji wa huduma za afya nyakati zote yaani usiku na mchana kwa ufanisi .
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa M. Mkwazu baada ya kuwapokea wageni kutoka halmashauri rafiki ya Enzkreis iliyopo ujerumani wakiwa na lengo la kukagua miradi ambayo inatekelezwa kwa ushirikiano kati ya halmashauri za masasi na ya enzkreis.
Mkwazu alisema katika ushirikiano huo wamekubaliana kutekeleza miradi ya utunzaji wa mazingira ambapo kuna miradi ya uwekaji umeme jua kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya na nyumba za watumishi ili kuboresha utoaji wa huduma za afya na utunza mazingira pamoja na matumizi ya biogas ambayo inatumia kinyesi cha wanyama kutengeneza nishati umeme kwa ajili ya mwanga, kupikia na matumizi mengine.
Pamoja na kwamba mradi huo utasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira lakini pia kwa halmashauri zetu tutakuwa tumetatua tatizo kubwa la umeme kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ambapo huduma hizi zitatolewa wakati wote yaani yakati za usiku na mchana tofauti na sasa ambapo baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya havina umeme, hivyo uwekaji wa umeme jua kwenye zahanati zetu ni utasaidia watumishi wa afya kuwahudumia wagonjwa wakati wote.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Gimbana Ntavyo alisema kuwa anaishukuru halmashauri ya enzkreis kwa misaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ambapo wameweza kuweka umeme jua eneo chumba cha maabara na chumba cha watoto njiti, ujenzi wa chumba cha uasuaji, uletaji wa vifaa vifaa na uboreshaji wa huduma za afya katika hospitali.
Aidha kutokana na ushirikiano baadhi ya wanamasasi wamehamasika kutumia m=nishatinishati ya Biogas kwa matumizi ya mwanga na kupikia kutokana urahisi wa gharama za kupata nishati hiyo ukilinganisha na umeme wa viwandani.
Kwa upande wake ndugu Mwita ambaye ametengeneza biogas nyumbani kwakwe kama njia ya kupata nishati ya umeme, na ameeleza kuwa umeme anaopata kupitia njia hiyo ni mwingi na hauna gharama kwani kinachohitajika nikuwa na mifugo inayoweza kuzalisha kinyesi kwaajili ya kukoroga tu.
“Napenda kuwahamasisha wananchi wa masasi na shemu nyingine kutengeneza mtambo wa biogas ili waweze kupata nishati ya umeme ya uhakika na kwa bei nafuu” alisema Mwita
Uwekaji wa umeme jua katika zahanati umeanza na utoaji wa mafunzo kwa vijana wa vijijini ili waweze kufanya kazi za uwekaji na matengenezo ya vifaa pale inapotokea tatizo kwa mda wa miaka mitatu lakini wakati huohuo wanaendelea kufanya shughuli za ufundi kwa watu walio nje ya mradi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa