Wananchi wa Halamashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wametakiwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwa kuchangia asilimia ishirini kama sheria inavyoelekeza ili kuepuka uwepo wa miradi viporo lakini pia kuhakikisha miradi inatekelezeka kwa wakati kama ilivyopangwa.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo bibi Changwa M Mkwazu wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo ili kuona utekelezaji wake kama unafanyika kwa kuzingatia viwango na mda uliopangwa na kujionea kuwa miradi mingi inachelewa kutokanana na wananchi kushiriki katika miradi hiyo kwa kusuasua.
Changwa alieleza kuwa halmashauri imejiwekea mpango wa kushirikisha wananchi kwenye miradi mingi ya ujenzi ambapo wananchi wanahusika kujitolea kufanya kazi zinazohitaji nguvu na nguvu kazi kama kusomba mchanga, kuchimba shimo au msingi kuchota maji na kusaidiana mafundi wakati wa kujenga lengo kiwa ni kuongeza umiliki wa mradi kwa jamii lakini pia kuipunguzia serikali mzigo wa kutekeleza miradi kwa asilimia mia moja.
Aidha katika ukaguzi huo miradi mingi haijakamilika kutokana na wananchi kutotimiza wajibu wao hali inayopelekea miradi mingi kutokamilika wa wakati alisema mkurugenzi
Changwa alisema “kuna haja ya kupita kila wakati kukagua miradi hii maana bila hivyo tatizo la miradi kutokamilika kwa wakati halitaishaisha, lakini pia watendaji wanaosimamia miradi hiyo watachukuliwa hatua kwa kushindwa kuhamasisha jamii kujitolea nguvu zao kwenye miradi”
Kwa uande wake Afisa Mipango wa halmashauri hiyo Ndugu Jeremia Lubeleje alisema kuwa watendaji ngazi ya kata na vijiji wanapaswa kufahamu kuwa wao ndio viongozi na wanatakiwa kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika miradi hiyo ili iweze kutumika kwani miradi inayokaguliwa sasa mingini ya ugenzi wa vyoo mashuleni hivyo ni mhimu ikakamilika haraka ili wanafunzi wawe na mazingira mazuri ya kusomea.
Lubeleje aliema kuwa kutokana na hali hiyo Baadhi ya miradi inàtekelezwa kwa kasi ndogo na haikamiliki kutokana na Jamii kutotoa mchango wao katika utekelezaji wa mradi.
Ni Vema jamii ikatambua Kuwa miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao ni kwa faida yao wenyewe hivyo ni bora kushiriki kikamilifu na kwa moyo ili miradi inàyotetwa iweze kukamilika na kuleta manufaa yaliyokusudiwa
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi, miradi ambayo ilikagualiwa ni ya ujenzi wa vyoo, madarasa, majengo ya afya, na majengo ya utawala ambayo imepelekewa fedha kwa mwaka 2016/ 2017 na ili kuona utekelezaji wake.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa