Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ameeleza kuwa Serikali ya Mkoa wa Mtwara inashirikiana na mradi wa "USAID Afya yangu" kanda ya kusini na wadau wengine kutoa elimu ya maambukizi ya UKIMWi pamoja na kuwaanzishia dawa wale waliobainika kuwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na wagonjwa wa kifua kikuu ambapo kwa sasa mpaka Septemba 2024 mkoa wa Mtwara una wagonjwa 35,934 ambao wanatumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (ARV).
Aidha ndani ya mwaka mmoja, wagonjwa 1,529 wa kifua kikuu wamepatiwa matibabu.
Kanali Sawala ameeleza hayo mapema tarehe 13 Dec 2024 wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa utoaji ruzuku wa USAID Afya yangu kwa mwaka 2025 baina ya USAID na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Halmashauri zote 9 za mkoa wa Mtwara, Hospitali ya Rufaa Mkoa-Ligula, Hospitali ya Rufaa-Ndanda.
Ameongeza kwa kusema kuwa mwaka huu 2024 mpaka Septemba 2025 mradi huu utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 3.56 kwaajili ya utekelezaji wa huduma za VVU na kifua kikuu ambapo fedha hizi zitaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti za vituo vya kutolea huduma za afya.
"Niwaombe viongozi kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha kwa kuzingatia taratibu za kiserikali na masharti ya mkataba mliosaini; kuandaa taarifa ya shughuli zote za utekelezaji wa mradi kwa wakati na kuziwasilisha kwa USAID; kuandaa shughuli na kuomba pesa za shughuli kwa wakati; kuhakikisha malipo yanafanyika kwa wahusika kwa wakati; kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma vina vifungu stahiki katika mipango yao." Alisema Kanali Sawala
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa