Serikali ya Tanzania imesaini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango Cha lami yenye urefu wa km 160 kutoka Mnivata, Tandahimba, Newala - MASASI, na ujenzi wa daraja la Mwiti na kampuni mbili za kichina.Ujenzi wa barabara hiyo, utagharimu kiasi Cha shilingi bilioni 234,512, fedha iliyotolewa kama mkopo na Benki ya Maendeleo ya Africa (AFDB)
Aidha mikataba hiyo imesainiwa Leo Juni 21,2023 katika viwanja vya Saba Saba Newala mjini mkoani Mtwara Kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kampuni ya china ya WU YI Company na China Communication Construction Company Limited.
Profesa Makame Mbarawa ni Waziri wa Ujenzi na uchukuzi ndiye mgeni rasmi ktk hafla hiyo ya utiaji saini ambapo amesema kwamba, Kampuni ya China ya Wu YI yenyewe inajenga kilomita 100 kutoka Mnivata hadi Mitesa kwa gharama ya shilingi bilioni 141.964 huku nayo Kampuni ya China Communication Construction Company Limited itajenga km 60 ya barabara hiyo kutoka Mitesa hadi Masasi kwa gharama ya shilingi bilioni 92.548./=
Waziri Mbarawa ameongeza kuwa, Ujenzi wa barabara hiyo ni manufaa makubwa kwa Wananchi kwasababu unakwenda kuwaondolea kero ya usafiri na hatmaye kuiboresha mitandao ya usafiri na usafirishaji na kukuza uchumi .
Hata hivyo pamoja na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya usaidizi ktk ujenzi huo pia amewaomba viongozi wote ambao wanapitiwa na mradi huo, Kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ambao wataanza kazi hiyo .
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa