Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mhe Fikiri Lukanga ameishukuru Halmashauri ya Enzkreis ya nchini ujerumani kwa msaada wao wa kuweka mifumo ya umeme Jua katika Zahanati 27 na nyumba za watumishi wa afya 51 lengo ikiwa ni kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa kwa akina mama wajawazito kwa kuwa na umeme wa uhakika muda.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mhe Fikiri Lukanga (mwenye shati jeusi) akizindua mfano wa sola katika tamasha la kuonesha teknolojia ya umeme jua katika kijiji cha Mijelejele wilayani masasi tarehe 13.08.2018
Lukanga ametoa shukrani hizo wakati wa tamasha la siku ya umeme jua lililofanyika katika kata ya Mijelejele wilayani humo liliolenga kuhamasisha wananchi juu ya kuongeza matumizi ya nishati ambayo ni rafiki wa mazingira na kusema kuwa anaipongeza wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala hasa umeme wa jua yanaongezeka.
Wananchi wa kijiji cha mijelejele wakifuatilia kwa makini matumizi ya vifaa vya umeme jua katika tamasha la kuonesha teknolojia ya umeme jua katika kijiji cha Mijelejele wilayani masasi tarehe 13.08.2018
Aidha Lukanga alifafanua kuwa nishati ya umeme ni kitu muhimu sana katika ustawi wa jamii kiuchumi na kijamii kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hivyo uwepo wa umeme wa wa uhakika ni uhakika wa maendeleo.
Marafiki kutoka Halmashauri ya Enzkreis Ujerumani wakisalimia wananchi kwenye tamasha la kuonesha teknolojia ya umeme jua katika kijiji cha Mijelejele
“Kila mtu ni shaidi kadhia kubwa zilizokuwa zinawapata akina mama wajawazito, watoto, wazee na wagonjwa kwa ujumla kutokana na kukosekana na nishati mbadala ya umeme katika zahanati zetu, hali hii inapelekea wauguzi wetu kutumia tochi za simu, vibatali na taa za chemli katika kutoa huduma nyakati za usiku” alieleza Satmah.
Fundi wa mfumo wa Umeme Jua akitoa maelekezo ya matumizi ya vifaa vya umeme huo katika tamasha la kuonesha teknolojia ya umeme jua katika kijiji cha Mijelejele wilayani masasi
Nae mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mhe Juma Satmah alieleza kuwa halmashauri za wilaya ya masasi Zinufaika sana na urafiki huo kwani pamoja na kuweka mifumo ya umeme jua pia wamekuwa wakifanya ziara za mafunzo kwa viongozi na wanafunzi lengo ikiwa ni kubadilishana mawazo lakini pia bado kuna mipango ya kufanya biashara pamoja ambapo watunaweza kupeleka bidhaa za masasi Ujerumani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mhe Juma Satmah akiongea wakati wa tamasha la kuonesha teknolojia ya umeme jua katika kijiji cha Mijelejele
“hii ni fursa adhimu sana kwa wanamasasi tunajivunia ushirikiano huu kati ya Masasi na Enzkreis ya Ujerumani kwani manufaa yake yananufaisha wananchi kwa ujumla” alisema Satmah
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu amesema kuwa kupitia mradi huu wa ufungaji wa mifumo ya umeme jua kwenye zahanati 27 hali ya utoaji wa huduma umeimarika sana ambapo wananchi wanapat huduma muda wote lakini pia wataalamu wa afya wanakaa nyumba ambazo zina umeme hali ambayo inawafanya wajione wako kwenye mazingira mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu akitoa neno kwa wananchi katika tamasha la kuonesha teknolojia ya umeme jua katika kijiji cha Mijelejele
Wakiongea kwa niaba ya wananchi wa masasi, wananchi wa mijelejele wameishukuru serikali kufanya tamasha hilo la matumizi ya nishati ya umeme jua kwani umeme nihuduma muhimu katika kufikia maendeleo ikiwemo ya afya , kiuchumi na kijamii kwa ujumla.
Mratibu waUshirikiano kati ya Masasi na Halmashauri ya Enzkreis Ujerumani Jeremiah Lubeleje akitoa ufafanuzi wa ushirikiano huo katika tamasha la kuonesha teknolojia ya umeme jua katika kijiji cha Mijelejele na kueleza kuwa kupitia Ushirikiano Huo zahanati 27 na nyumba 51 za watumishi wa afya zimefungwa mfumo wa umeme jua. aidha wanampango wa kufanya shughuli zingine za kimaendeleo.
Kwa upande wa Mwakilishi wa wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) Emanuela Laswahi alisema kuwa TAREA iko tayari kuhamasisha wananchi kutambua umuhimu wa kutumia umeme Jua na Nishati nyingine Jadidifu kwa lengo la kulinda mazingira,kuinua uchumi na kuboresha huduma za jamii kwa ujumla, hivyo “tunasisitiza wananchi waongeze kazi ya utumiaji wa nishati Jadidifu maana ni rafiki wa mazingira”
Naibu Katibu Mkuu wa TAREA bibi Emanuela Laswahi akieleza jambo kwa wananchi wa Mijelejele
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa