Halmashauri ya Wilaya Masasi leo julai 31/2024 imefanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri hiyo huku Uchaguzi huo sasa umeongeza matumaini makubwa ya kiutendaji katika kusimamia utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Halmashauri katika Mwaka mpya wa fedha 2024/2025.
Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Chigugu Bi.Amina S.Mpandula amechaguliwa tena kuendelea kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kura za ndio 38 zilizopigwa, Kati ya Wajumbe 43 wa baraza la Madiwani ambao walikuwepo, na Wajumbe 3 hawakuwepo Kabisa kutokana na udhuru mbalimbali.
Edith Shayo mwakilishi Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akitangaza matokeo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi Fatma Kubenea, amesema kanuni ya uchaguzi inaelekeza vyama vya Siasa kupeleka majina ya wagombea wao lakini mpaka sasa anabarua Kutoka Chama kimoja tu Cha Mapinduzi (CCM) na barua hiyo ilikuwa ni ya tarehe 29/07/2024 inayohusu uwasilishaji wa jina la mgombea kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Amesema jumla ya Wajumbe wote wa baraza ni 46, "na waliohudhuria kwa leo wapo 43, na wajumbe waliopiga kura ni 38, na kura zote ni za ndio, na hakuna kura iliyoharibika wala kura ya hapana, hivyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Wilaya Masasi napenda kumtangaza Bi.Amina Mpandula kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri"
Kwaupande wake Bi.Amina S.Mpandula ambaye ndiye mshindi kwa nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti ameendelea kuwashukuru Wajumbe wote ambao bado wameendelea kumchagua tena kuendelea na nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti na hivyo anahaidi kufanya nao kazi kwa pamoja ili kuendelea kuipatia Maendeleo Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni ya uendeshaji wa vikao vya Halmashauri zilizotangazwa kwenye gazeti la Serikali na.252 la tarehe 28/07/2017 kupitia kanuni ndogo 6,1A zinazoelekeza kuwepo kwa baraza la mwaka ambapo moja ya majukumu yake ni kufanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti pamoja na Shughuli nyinginezo.
Na.Winifrida Ndunguru
........Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa