Kamati ya Siasa (CCM) Mkoa wa Mtwara leo tarehe 08/01/2025 imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama hicho (CCM) kwa kutembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Ziara hiyo ambayo ni ya siku moja katika Halmashauri hiyo awali imetembelea na kukagua ujenzi wa vyumba 24 vya Madarasa na matundu 14 ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Mpeta ambayo inatekelezwa kwa njia ya Force account ambapo hadi sasa tayari ujenzi huo umekamilika na Shughuli iliyobaki ni ukamilishaji wa viti na meza 960.
Akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa mradi huo mbele ya Kamati hiyo ya Siasa Mkoa, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mpeta Mwalimu Rajab Bakari Nampoto amesema Shule ya Sekondari Mpeta ilipokea shilingi 594,000,000.00 mnamo tarehe 30/03/2024 kutoka Serikali kuu kupitia fedha za ruzuku ya miradi ya Maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 24 vya Madarasa na matundu 14 ya Vyoo, ambapo mradi ulianza kutekelezwa tarehe 25/04/2024 na ulitakiwa kukamilika tarehe 19/07/2024.
"Mradi umepitia changamoto ya ukosefu wa Maji na mbao kwa ajili ya kukamilisha viti na meza za wanafunzi, Lakini kwa kushirikiana na Viongozi pamoja na Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri na TFS wameendelea kushughulikia utatuzi wa mbao kwa ajili ya viti na meza" alisema mwalimu Nampoto
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara Ndg.Said Nyengedi amesema anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na mapenzi makubwa na Watanzania na hasa Wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa Kutoa fedha nyingi ambazo zimewezesha kujengwa kwa mradi huo.
" Fedha alizotoa kwenye mradi huu ni nyingi sana, haya ni mapenzi kwetu,.vijana wetu wanakuja kusoma kwenye mazingira mazuri sana ambayo sisi wengine hatukusoma kwenye mazingira kama haya, hatuna budi kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi, kumuunga mkono mhe.Rais wetu, Lakini tuna kila sababu ya kukiunga Chama chetu Cha Mapinduzi kwa mambo makubwa yanayofanyika katika nchi Lakini katika mkoa wetu na moja wapo ni hili ".
"Mradi huu utekelezaji wake kwakwelii tumefurahishwa na tumeupokea kwa mikono miwili hivyo niwaombe muitunze Miundo mbinu ya shule hii, ni ya kwenu Wananchi wa mpeta, Serikali imewajengea na nyinyi sasa Katika kuitunza miundo mbinu hii mnatakiwa kuhakikisha mnapanda miti.
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mapokezi kwa Kamati hiyo kwenye mradi huo wa vyumba 24 vya Madarasa na matundu 14 ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Mpeta wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo ambao una tija kubwa kwao.
Shule ya Sekondari Mpeta ilisajiliwa rasmi tarehe 17/11/2022 ikiwa na namba ya usajili S.5936, ina Jumla ya wanafunzi 467 ambao wasichana ni 242, wavulana ni 225 kati Yao wanafunzi wa kidato cha,I_III ni 222 na kidato cha IV - VI ni 245.
08/01/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa