Timu ya kuandaa mpango wa kituo Cha kutolea huduma za Afya ya Msingi imetakiwa kuandaa mpango kwa kuzingatia vipaumbele, malengo na kuanisha kazi zitakazofanyika ili kutimiza malengo na kupata matokeo tarajiwa.
Aidha timu hiyo pia imetakiwa kabla ya kuandaa makisio ya bajeti ni vyema katika Kila kituo Cha kutolea huduma za Afya ya Msingi ziwe na Kamati ya usimamizi wa kituo ambayo itahusishwa katika kuandaa mipango, kuelekeza, kusimamia na Kutoa taarifa ya namna rasirimali za vituo zinavyotumika.
Hayo yamesemwa Leo tarehe 11/12/2024 na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Dkt.Ruben Mwakilima katika kikao cha maandalizi ya Mipango ya vituo vya kutolea huduma za Afya ya Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambacho kimefanyikia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo mbuyuni Masasi, huku ajenda mbalimbali zikijadiliwa ikwemo mapito ya maandalizi ya Mipango ya vituo, kupitia vigezo vya kuzingatia kuandaa mipango, kupitia taarifa ya Mapato kuanzia jan- Novemba 2024 pamoja na mijadala mbalimbali juu ya Mipango ya vituo.
"Mchakato wa uandaaji wa mpango wa kituo unapaswa kuwa shirikishi, na mpango huo ulioandaliwa utapitishwa na kupewa baraka na Kamati ya usimamizi ya kituo husika kabla ya kupelekwa na kuingizwa kwenye mpango kabambe wa Afya wa Halmashauri , wakati huo huo timu ya uandaaji wa Kituo Cha kutolea huduma za Afya ya Msingi inatakiwa kuweka bajeti ya mafunzo kwa Watumishi wa Kituo kwenye mpango wake kulingana na mahitaji yake, huku CHMT itakuwa na jukumu la kuratibu mafunzo haya kupitia mpango na bajeti yake."...alisema Mwakilima
Ameongeza kuwa vituo vya Afya ni hatua ya kwanza ya rufaa kwa Zahanati na vinajukumu la kusimamia zahanati zinazovizunguka, hivyo ni muhimu mpango wa vituo vya Afya kuweka bajeti ya usimamizi katika zahanati.
" Namna ya kuandaa bajeti na vyanzo vya Mapato ya kituo ambapo yapo Maeneo muhimu sita ya kuzingatia unapoandaa bajeti ni kipaumbele, Afua, malengo/Lengo, Maeneo yanayokusudiwa, kazi zitakazofanyika na matokeo/ufanisi."
Hata hivyo Mwakilima amehitimisha kwa kusema kwamba timu ya uandaaji wa mpango inatakiwa Kutoa maelezo ya idadi ya vijiji/mitaa, Kata zinazohudumiwa na kituo Cha kutolea huduma za Afya, idadi ya wahudumu wa Afya katika ngazi ya Jamii kwenye eneo linalohudumiwa na kituo husika na idadi ya majina ya Zahanati/ vituo vya Afya vinavyohudumiwa na kituo Cha Afya au Hospitali ya Wilaya, Shughuli za uchumi katika Eneo husika.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa